Vijana kama kawaida 2020 tufanye kweli

Mwakaboko King

JF-Expert Member
Apr 22, 2015
1,099
207
Ni ukweli usiopingika kuwa kundi la vijana katika nchi yoyote ile linabaki kuwa kundi muhimu katika kusukuma ajenda mbalimbali. Mwaka 2015 wakati wa Uchaguzi Mkuu vijana tulikuwa mstari wa mbele katika nyanja zote kwa maana ya Michakato ya kuwapata wagombea, Kampeni za Vyama vya Siasa, Uchaguzi wenyewe na hata baada ya kutangazwa washindi wa uchaguzi vijana tuliingia barabarani kuwapongeza washindi kwa maandamano, kucheza na shangwe za kila aina.

Nimeandika uzi huu kwa lengo moja tu kwamba kama tulivyofanya 2015 kwa kutambua wajibu wetu kama vijana tufanye kweli 2020 kwenye uchaguzi Mkuu kwa kuhakikisha tunawachagua viongozi wenye sifa. Pia sisi vijana ambao ni kundi kubwa kuelekea uchaguzi ujao tuwe walinzi wa amani yetu kwa kushiriki kikamilifu katika hatua zote kama tulivyofanya 2015.

Vijana tujitokeze kwa wingi kuwania nafasi za uongozi wa kisiasa, tuingie kwenye hizo nafasi kwa kuwa uwezo wa kuongoza tunao, sababu za kuongoza tunazo na nia tunayo! Zaidi ya yote vijana tunao wajibu wa kujitokeza kupiga kura mwaka 2020 zaidi ya vile tulivyofanya mwaka 2015, tuhakikishe tunashiriki moja kwa moja katika kuwaweka madarakani viongozi tunaowataka.

Mwisho kuelekea uchaguzi ujao, kwa mujibu wa majukumu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutakua na zoezi la uboreshaji wa Daftari la Wapiga kura ili kuwapa fursa wananchi wengi zaidi hasa waliofikisha umri wa miaka 18 waweze kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu ujao, chonde chonde vijana tuitumie vizuri fursa hii, naamini tutajitokeza kwa wingi kuhakiki taarifa zetu na wale wasiokuwa na Kadi za kupigia kura ambao watakuwa wametimiza umri watawezeshwa kuwa na kadi hizo ili wapige Kura.

Vijana ndio sisi, Kama kawaida 2020 ni mafuriko ya kwenda kupiga Kura, Hakuna kulala!
 
IMG_20170226_180142.jpg
 
Sijakuelewa una maanisha vijana kina TID,Wema na wengineo?otherwise achana na porojo za viroba maana vijana hawakuweza kufanya lolote ktk uchaguzi ule ndo maana leo hii wengi wanajuta kwa chaguo walizofanya.Wengine walitumika kama toilet paper,wlikuwa wanaitwa IKULU 2015 mwaka huu 2017 wanaitwa SENTRO YA POLISI KANDA MAALUMU YA DASALAMU kwa Amri ya mtukufu wa mkoa aliyegoma kumiliki vyeti.
 
Mkuu vijana wa Tanzania sio TID na Wema!! Na image ya vijana unayoifikiria sio hiyo, think out of the box! Tanzania kuna vijana wengi sana wana akili na wanajitambua na wanajua kufanya maamuzi sahihi! Mtoa post kajaribu kuonesha umuhimu wa vijana katika kushiriki chaguzi kwa Amani na Utulivu na kujitokeza kwa wingi siku ya Uchaguzi 2020!

Matokeo ya maamuzi yao baada ya kupiga kura 2015 hayahojiwi na mtu yeyote!
 
Ni kweli wapo wengi wenye akili lakini hawajitambui easily to be civilised and corrupt
 
Barani Africa Tanzania inaongoza kwa kuendesha chaguzi Huru na za Haki
Ahaaaaaa mr Jecha s Jecha unamjua????yaaani Jecha kawazidi Ghana na Nigeria??
Sijakuelewa una maanisha vijana kina TID,Wema na wengineo?otherwise achana na porojo za viroba maana vijana hawakuweza kufanya lolote ktk uchaguzi ule ndo maana leo hii wengi wanajuta kwa chaguo walizofanya.Wengine walitumika kama toilet paper,wlikuwa wanaitwa IKULU 2015 mwaka huu 2017 wanaitwa SENTRO YA POLISI KANDA MAALUMU YA DASALAMU kwa Amri ya mtukufu wa mkoa aliyegoma kumiliki vyeti.
 
Vijana tuna hasira na ajiraaaaaaaa .2020 lazima tumuweke madarakani mtu wakutupa ajira na mkopp
 
Back
Top Bottom