mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,227
- 6,666
Makala yenye kichwa cha habari hapo juu imeandikwa kwenye gazeti la Nipashe, Alhamisi Februari 15, 2017.
Naileta humu jamvini kukumbushana ili kila mmoja wetu aweze kujipima na kuchukua tahadhari dhidi ya maisha yanayohatarisha afya yake.
Hakika kama unakidhi vigezo hivi, endelea na jinsi ya maisha yako hayo hayo, la badilika, ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi, kwa ajili ya afya ya mwili.
1) UMRI WA MIAKA 20 , kama unaweza:
- kuweza kukimbia 5km kwa dakika 30;
- kujinyoosha kwenye ubao bila kuulalia kwa dakika moja;
- kuchuchumaa, kunyanyuka, kuruka mara 20 akiwa kwenye mstari bila ya kupumzika.
2) UMRI WA MIAKA 30 , kama unaweza:
- kukimbia maili moja katika muda wa chini ya dakika 9;
- kujinyoosha kwenye ubao bila kuulalia kwa sekunde 45;
- kunyanyua mzigo ulio nusu ya uzito wako bila ya kusaidiwa na kitu chochote ukiwa umesimama.
3) UMRI WA MIAKA 40 , kama unaweza:
- kukimbia kwa kasi kwa sekunde 60 bila ya kusimama;
- kugusa viatu vyako ukiwa umenyoosha miguu yako bila ya kuikunja;
- kupiga 'pushapu' mara 10 bila ya kusimama.
4) UMRI WA MIAKA 50 , kama unaweza:
- kukimbia kwa kasi ya wastani kwa sekunde 60 bila ya kusimama;
- kuchuchumaa, kunyanyuka, kuruka mara tano kwenye mstari bila ya kupumzika;
- kukaa kwa kukunja miguu yako na kusimama tena bila ya kutumia mikono yako.
5) UMRI WA MIAKA 60 , kama unaweza:
- kutembea zaidi ya hatua 10,000 kwa siku;
- kuchuchumaa na kunyanyuka mara 12 bila ya kupumzika.
6) UMRI WA MIAKA 70 , kama unaweza:
- kutembea umbali wa maili moja chini ya dakika 16;
- kupanda ngazi kwa hatua 10 bila taabu katika kipindi cha sekunde 30;
- kunyanyuka toka kwenye kiti bila ya kutumia mikono na kurudia tena walau mara 12 katika kipindi cha sekunde 30.
Jipime kama uko imara na timamu, kiafya. Anza na endelea na mazoezi hayo kila mara, hasa asubuhi na jioni, kabla ya kuoga, na baadaye upate mlo ulio kamili.