Mkuu binadamu asili yake ilikuwa uwindaji, fikiria ile unaamka asubuhi inabidi uanze kutafuta chakula, unahangaika porini ukiona matunda unakula, hatimae nyama inapatikana inachomwa unakula, mwili unauwezo wa kuhifadhi chakula kwa mahitaji ya siku chache zijazo kama utakosa chakula katika uwindaji.
Mambo yamebadilika, siku hizi unaamka asubuhi mkate, mziwa, mayai nk viko kwenye jokofu, unawasha birika unachemsha chai, unaweka sukari na maziwa, mkate unapaka butter na jam, ukimaliza unaangalia TV. Ule uwezo wa mwili kuhifadhi chakula kwa siku chache unauzidishia kazi ya kuhifadhi chakula ambacho kimebadilishwa kuwa mafuta ambayo hayatakaa yatumike kwani kila siku unaongeza chakula.