Vietel/ Halotel vs TTCL

Vietel/ Halotel vs TTCL

kipoke KIPOKE

Member
Joined
Apr 20, 2015
Posts
54
Reaction score
9
Hii naona kama comedy hivi Pinda mtoto akiugua unatafuta mwingine?

Ni swali ambalo watanzania wengi sana tunajiuliza tuna kampuni kubwa sana za mawasiliano nyingi zikiwa za watu binafsi na nyingine kubwa ambayo inasuasua TTCL Ni ya serikali leo waziri mkuu anawakaribisha wawekezaji wanaofanya same business na TTCL SASA NIA YAKE NI NINI ?Kama haifanyi vizuri ni bora ikafutwa ndio ulete kampuni nyingine ya serikari.

Sisi tunataka huduma safi na bora ila tunahoji je serikali inaweza ikatumia wawekezaji kwenye mawasiliano ya nchi?maana kwa kuazia halotel wamepewa shule karibia laki tatu hospitali zote vijiji vyote wameweka minara tena mingine wanatumia ya TTCL
 
Halotel wanatufaa sana maana hawa wengine wameshindwa kutoa huduma bora vijijini
 
Ongea ueleweke maana hapa watu yawezekana ukawa ujaeleweka!
 
Kuja kwa halotel inaweza pia kuiboost ttcl
Stay calm and watch
 
Kampuni ni yake kwa % kubwa na lengo lake kuiua TTCL labda anadhani hatujui kama ana hisa nyingi huko,,
na ndiyo mjue kuwa ni jinsi gani serikali iliyoko madarakani ilinyodhamiria kuua makampuni yaliyoko Tanzania, lakini tutafika tu
 
Kama wanaweka minara vijijin ambako hamna network con tatizo
 
Kampuni ni yake kwa % kubwa na lengo lake kuiua TTCL labda anadhani hatujui kama ana hisa nyingi huko,,
na ndiyo mjue kuwa ni jinsi gani serikali iliyoko madarakani ilinyodhamiria kuua makampuni yaliyoko Tanzania, lakini tutafika tu
Ndio maana kuna kipindi safari zake za Vietinam zilikua haziishi! Aliwahi kusema siku moja wakati wa hafla ya kuchangia madawati kua alienda Vietinam akapewa vizawadi ndio maana alichangia hela nyingi kwenye hafla hiyo! Hapa hakuna cha Mtoto wa mkulima wala nini! Fiksi tupu.
 
Hiyo inaitwa Publc private partnership (PPP).K:ama mchakato wa manunuzi wa PPRA umefuatwa binafsi sioni tatizo hata kidogo.
 
Hiyo ndiyo Tanzania. Nchi isiyokuwa na alama. Twiga wanapelekwa nje, hakuna shirika la taifa la ndege, hakuna shirika imara la reli tunajenga barabara halafu zinaharibiwa na malori, hatuna shirika imara la taifa la simu nk, nk.
Viongozi wetu hawajifunzi. Maraisi wote wa Marekani waliotembelea Tz waliitumia Ttcl kwa mawasiliano yao. Bila shaka waliamini kuwa kutumia kampuni ya serikali ni salama na ni heshima kwa taifa husika. Miaka zaidi ya hamsini ya uhuru wetu bado watalii wanashuka Nairobi kwa ajili ya kuuona/ kupanda mlima Kilimanjaro.
Kwa mtindo huu hata mkongo wa taifa ambao juzi nilimsikia Kikwete akijisifia kwa kuujenga na ambao unasimamiwa na Ttcl kwa niaba ya serikali hautakuwa na manufaa na umepata chachu ya kuzidi kuhujumiwa.
Zimebaki siku 6.
 
Kampuni ni yake kwa % kubwa na lengo lake kuiua TTCL labda anadhani hatujui kama ana hisa nyingi huko,,
na ndiyo mjue kuwa ni jinsi gani serikali iliyoko madarakani ilinyodhamiria kuua makampuni yaliyoko Tanzania, lakini tutafika tu

ikiwa hujui bora kukaa kimya Halote/Vietell ni kampuni ya Jeshi la Vietnam
 
Hii naona kama comedy hivi Pinda mtoto akiugua unatafuta mwingine?

Ni swali ambalo watanzania wengi sana tunajiuliza tuna kampuni kubwa sana za mawasiliano nyingi zikiwa za watu binafsi na nyingine kubwa ambayo inasuasua TTCL Ni ya serikali leo waziri mkuu anawakaribisha wawekezaji wanaofanya same business na TTCL SASA NIA YAKE NI NINI ?Kama haifanyi vizuri ni bora ikafutwa ndio ulete kampuni nyingine ya serikari.

Sisi tunataka huduma safi na bora ila tunahoji je serikali inaweza ikatumia wawekezaji kwenye mawasiliano ya nchi?maana kwa kuazia halotel wamepewa shule karibia laki tatu hospitali zote vijiji vyote wameweka minara tena mingine wanatumia ya TTCL

Hueleweki kabisa.
 
Hiyo inaitwa Publc private partnership (PPP).K:ama mchakato wa manunuzi wa PPRA umefuatwa binafsi sioni tatizo hata kidogo.
Mkuu ni kweli inaweza isiwe tatizo, lakini ujue kuwa serikali ilinunua mkongo kwa kampuni ya sea com, katika nchi mojawapo huko Ulaya tena kwa gharama kubwa, na ndiyo maana hata hawa provider wengine kama voda, tigo nk wamepitishia data zao katika huo mkongo wa Taifa. sasa iweje halotel wao waruhusiwe kununua huko huko sea com ambako serikali imenunua na private provider nao wanunue huko?
je kuna haja gani ya serikali kuruhusu kampuni binafsi iwekeze kwa kununua mkongo huko? kama kweli wana nia nzuri na nchi hii kwa nini asiwekeze mawasiliano yake kama provider wengine?
 
Hayo matatizo ya mawasiliano Lowassa atayashughulikia.Mpeni kura zote za ndio,msahau malalamiko ya kuhujumiwa kwa mashirika ya UMMA.
 
Back
Top Bottom