Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,814
- 34,196
Chupa za Vidonge vya kuongeza nguvu za kiume Viagra.
Stori: Mwandishi, Wetu Wikienda
Dar es Salaam: Wamekwisha! Imebainika kuwa watu wanaotumia vidonge vya kuongeza nguvu za kiume vya Viagra huku wakiwa na matatizo ya moyo na wengine kuchanganya na pombe wapo kwenye hatari ya kupoteza maisha kama ripoti za madaktari zinavyoeleza, Ijumaa Wikienda lina ripoti kamili ambapo watu 86 wamepoteza maisha nchini Uingereza kwa matumizi ya vidonge hivyo.
Mwalimu na Naibu Waziri Wake Dr Hamisi Kigwangallah.
UCHUNGUZI WA WIKIENDA
Uchunguzi wa Ijumaa Wikienda umebaini kwamba vidonge hivyo kwa sasa hapa nchini vinatumiwa sana na baadhi ya wanaume au vijana wengi kwa lengo la kuongeza uwezo wao wanapokuwa faragha na wapenzi wao.
Ilibainika kwamba vidonge hivyo hutumiwa zaidi na wanaume wasiomudu kufanya tendo la ndoa ili kuwawezesha kukidhi haja zao au za wenza wao.
Vidonge vya kuongeza nguvu za kiume vya Viagra.
KUKOMOA?
Lakini vidonge hivyo vimekuwa vikitumiwa na vijana wengi kwa lengo la kumkomoa mwanamke au wengine hufanya kwa kuiga kutoka kwa waigizaji wa video za ngono (pornograph).
CHANZO CHA WANAUME KUFIA GESTI
Uchunguzi huo ulibaini kwamba kumekuwa na wimbi la wanaume kufia gesti wakiwa na wanawake mara tu baada ya kutumia vidonge hivyo na kushushia na pombe, jambo linalowasababishia mshtuko wa moyo.
KISA NA MKASA
Akizungumzia tukio la kusikitisha la rafiki yake aliyefariki akiwa gesti na mwanamke, mfanyabiashara mmoja wa jijini Arusha aliyejitambulisha kwa jina moja la Lyimo alikuwa na haya ya kueleza:
“Nilikuwa na rafiki yangu (anamtaja jina). Aliambiwa na demu wake kuwa hawezi kumtosheleza wanapokuwa faragha. Alichokifanya rafiki yangu ni kutafuta vidonge hivyo bila ushauri wa daktari.
“Ulipofika muda wa tendo la ndoa akiwa na demu wake gesti si ndiyo akameza vidonge?
“Kumbe jamaa yangu alikuwa na presha. Kilichofuata ni kwamba alifariki dunia kabla ya kumfikisha hospitalini na kweli ripoti ilionesha kwamba alimeza Viagra na pombe na hivi sasa hatunaye.”
WATAALAM
Wataalam wanaeleza kuwa vidonge hivyo husababisha kuganda kwa damu hivyo kumweka hatarini mtumiaji ambaye hupoteza maisha kwa shambulio la moyo na kiharusi.
Kwa mujibu wa kitengo cha kusimamia madawa cha Medicine Control Agency cha nchini Uingereza, wanaume wapatao 86 waliokuwa wakitumia vidonge hivyo kati ya mwaka 1998 hadi sasa wamepoteza maisha kutokana na madhara yake kwenye moyo.
UTAFITI MPYA
Utafiti mpya unaonesha kuwa vidonge hivyo vinazidi kuongeza vifo vya mshtuko wa moyo kwa wagonjwa ambao tayari wana magonjwa ya moyo.
Dokta Xiaoping Du ambaye ni mfamasia wa Chuo Kikuu cha Chicago College of Medicine, anasema: “Viagra peke yake haviwezi kusababisha shambulio la moyo kwa mtu mwenye afya (ambaye haumwi) lakini utafiti wetu unaonesha kuwa hilo linawezekana kwa mtu ambaye tayari ana dalili za ugonjwa wa moyo.”
Wataalam wanaeleza kuwa vidonge hivyo haviruhusiwi kabisa kwa mwanaume mwenye matatizo ya moyo.Vidonge hivyo vinakadiriwa kutumiwa na watu milioni 20 duniani kote ingawa msisitizo upo kwenye kufuata ushauri wa daktari.
MBALI NA KIFO
Mbali na kusababisha kifo kwa shinikizo la damu, pia matumizi makubwa ya vidonge hivyo hufanya tatizo la nguvu za kiume kuwa kubwa zaidi kwa sababu humfanya mtu ‘kupafomu’ tendo kwa muda tu na anapohitaji tena humpasa kumeza tena.
Hali hiyo humfanya mwanaume kuwa dependant (tegemezi) na kumfanya azidi kuongeza dozi zaidi na mwishowe hutengeneza sumu mwilini na kuua kabisa nguvu za kiume.
Madhara mengine ni kupoteza uwezo wa kusikia na kuona.
Gazeti hili lilimtafuta Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kigwangalla ili kujua kauli ya serikali juu ya vidonge hivyo lakini simu yake haikuwa ikipatikana hewani.
Vidonge vya nguvu za kiume vyaua watu 86