Ni kweli kwamba Flagly (Metronidazole) ile ya njano inazuia mimba kuingia?

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Feb 26, 2024
4,801
9,785
Heshima kwenu nyote

Ni wazi kuwa sie wabongo ni watu wa kujaribu vitu hata vile tusivyo visomea.

Nitaweka baadhi ya dawa(vidonge) ambavyo vinatibu ugonjwa fln lakni Kwa ujuaji wa kibongo vidonge hivo hutumika Kwa matumizi mengine na kuleta manufaa.

Baadhi ya vidonge Hivi ni kama(sitatumia majina ya kitaalamu Bali yetu tuyajuavyo kitaa)

Indosini:- Hiki kidonge amini usiamini pamoja na kutibu binadamu pia ni SUMU nzuri sana Kwa panya.

Kidonge hiki ukichukua tembe1 ukaisaga na kuchanganya na chakula anachokula panya lazima panya atakufa tu.

Septrini:-Hii ikisagwa na kuchanganya kwenye mafuta ama lotion hutibu MBA!!

Kuna Ile dawa hupewa wagonjwa wa ukoma(jina nimesahau)

Hiyo dawa ikisagwa na kuwekwa kwenye kidonda hupona na kukausha kabisa Tena Kwa muda mfupi.

Doxy:- hii hutibu kuku anayeumwa

Zipo dawa nyingi sana zinazotumika tofauti na kuleta faida(kuponya)

Hivyo najua wazi kuwa flagly hutibu hasa tumbo la kuhara nk.

Kuna hii nimekuwa nikisikia kwa siku nyingi kuwa flagly ya njano akipiga Kwa mkupuo 4 baada ya tendo basi hata kama alikuwa kwenye siku za hatari mimba haiwezi ingia je Kuna ukweli wowote ule kuhusu hili?

Naamini wajumvi wa mambo humu wapo wa kutosha.

Karibuni
 

Attachments

  • 20240707_094520.jpg
    20240707_094520.jpg
    93.7 KB · Views: 6
Acha tu mtoto azaliwe, mimi nitakusaidia kulea mkuu. Usipende kuuwa watoto wasiokuwa na hatia.

Jifunze kwa mama Diamond na wengine waliokomaa kulea watoto wao wenyew, na leo hii wanakula faida ya malezi yao.
 
Back
Top Bottom