MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Ni video inayosikitisha sana kiasi kwamba hata baadhi ya wananchi katika mkutano walionyesha sura za masikitiko huku wengine wakitoa machozi.
Rais Magufuli baada ya kusikiliza kilio na malalamiko ya Mama, ilibidi aseme, '' Nimejifunza mengi kuhusu yanayoendelea hapa Hanang. Hizi kero zilizozungumzwa hata angekuwa shetani angesikitika''.
Rais aliamulu wale wote waliomtendea vitendo vya kinyama, wakamatwe haraka na vyombo vya kusimamia sheria ili haki itendeke.
Rais akawaagiza viongozi angalau watenge siku maalum kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia majibu au ufumbuzi wa haraka.
Rais alisema ni aibu sana kwa Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa wilaya kushindwa kutatua kero za wananchi ambazo ziko ndani ya uwezo wao.
Rais alimaliza kwa kuwaomba wananchi wawe wavumilivu kwa kipindi kifupi kwa sababu serikali yake inajipanga kuhakikisha inaondoa kero kama hizi ambazo zimebainisha na Mama ambaye kwa uchungu ametoa machozi.
Rais alitoa kiasi cha pesa kutoka mfukoni mwake na kumpatia Mama ili zimsaidie wakati tatizo lake likipata ufumbuzi wa kudumu.
Kwa wenye Megabyte (Mb) ndogo, unaweza kuangalia kuanzia kwenye dakika ya 13:20.