- Source #1
- View Source #1
kumekuwepo na video hi inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii husasani facebook na tiktok je ukweli wa video hii ni upi?
- Tunachokijua
- Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kumekuwa na kipande cha video kinqchosambazwa na watumiaji mbalimbali kikionesha watalii wakiwa mbugani na mmoja wao anabebwa na Twiga.
Je, video hiyo ni halisi au imetengenezwa kwa Teknolojia ya Akili Unde?
JamiiCheck imefuatilia na kubaini kuwa video hiyo si halisi bali imetengenezwa kwa teknolojia ya akili unde.
Video hiyo ina mapungufu kadhaa ikiwemo si rahisi Twiga kumbeba binadamu mkubwa hivyo na kukimbia naye kwa kasi kubwa.
Aidha kwa kutumia nyenzo za kidigitali ikiwemo ya Hive Moderation, JamiiCheck imebaini kuwa video hiyo imeundwa kwa AI kwa takribani 99%.