Victorie Inghabire adai msamaha wake umetokana na shinikizo la Wazungu; Kagame atokwa povu zito !

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,650
218,126
Mwanamama mashuhuri wa Rwanda ambaye pia ni kiboko ya Kagame Victorie Inghabire amedai kwamba msamaha wake wa kutoka gerezani haukutokana na Huruma ya Dikteta Kagame , bali ulitokana na shinikizo la kimataifa.

Hata hivyo kauli hiyo imemkasirisha Kagame ambaye amedai kwamba mwanamama huyo akizidisha kiherehere atarejeshwa tena lupango au atafukuzwa nchini Rwanda , Kagame ameyasema hayo wakati akilihutubia bunge butu la Rwanda ambalo " lilichaguliwa " septemba 3 mwaka huu.

Kagame ambaye ndio Rais anayeongoza kwa kuwaogopa wanasiasa wa upinzani wanawake duniani , amedai kwamba hajawahi kupokea shinikizo lolote kuhusiana na msamaha wa wafungwa .

Mytake : Rwanda itakombolewa na wanawake .
 
Yanakuja kwetu bongo. Bunge la ccm. Manake 2020 sioni mbunge wa upinzani mjengoni.
Jiwe ataongeza siku za kuishi Ikulu atakavyo na hakuna ccm yyte atapinga. Hata usiposema “ndiyooo” itakuwa ndo Ndiyooo.
Tusubiri bunge la hovyo ambalo halijawahi kutokea ktk maisha ya Mtanzania yyte yule awe hai au waliotangulia mbele ya haki.
 
Mwanamama mashuhuri wa Rwanda ambaye pia ni kiboko ya Kagame Victorie Inghabire amedai kwamba msamaha wake wa kutoka gerezani haukutokana na Huruma ya Dikteta Kagame , bali ulitokana na shinikizo la kimataifa.

Hata hivyo kauli hiyo imemkasirisha Kagame ambaye amedai kwamba mwanamama huyo akizidisha kiherehere atarejeshwa tena lupango au atafukuzwa nchini Rwanda , Kagame ameyasema hayo wakati akilihutubia bunge butu la Rwanda ambalo " lilichaguliwa " septemba 3 mwaka huu.

Kagame ambaye ndio Rais anayeongoza kwa kuwaogopa wanasiasa wa upinzani wanawake duniani , amedai kwamba hajawahi kupokea shinikizo lolote kuhusiana na msamaha wa wafungwa .

Mytake : Rwanda itakombolewa na wanawake .
Umeandika kishabiki zaidi. Mungu nibariki.
 
Kagame mbele ya wanawake ni kama mkate ukitiwa ndani ya chai.
Ikumbukwe amewaweka wengi sana bungeni. Na urefu wote ule ukimtishia demu utajua hajui.
Yaani ni kama mjeshi asiyejua kutongoza ila mkali vitani.
 
Back
Top Bottom