Vichekesho

Kabwe94

Member
Joined
Feb 18, 2014
Posts
6
Reaction score
1
Mfano ;- wewe
umempenda demu ,,
ukamtongoza akakubali ,,
akakuambia uje
nyumbani ,, ukafika kwao
ukamuuliza ,, unakaa na
nani '? akakujibu :- naishi
na bibi ila hayupo hapa
yupo hospitali kalazwa ,,
mkalala kitandani ,,usiku
wa manane mara mkasikia
hodi ,, Binti akakuambia
jifiche uvunguni '
ukajificha" akafungua
mlango ,, akakuta watu
wameleta maiti ya bibi
yake ,, wakaja kuiweka
kitandani ,, huku wewe
ukiwa umejificha chini ya
uvungu wa kile kitanda
mpk asbh ,, ukicheki watu
kibao wamejaa sebuleni
mpaka nje ,, je !
utafanyaje na nguo kalalia
marehemu '? nipe jibu
fasta.
 
Najifanya mzimu. Nachomoka huko uvunguni nikiwa nimekunja sura nionekane kama zombi. Ile wansshangaa tu na-grab kanga ya muombolezaji mmojawapo najitupia kiaina ili sura isionekane vizuri afu natoka kwa mwendo huohuo wa kizombi zombi (ghost walk) nikichemka basi bahati mbaya...
 
hahahha.nimepata picha ya nwendo wa kizombi ulivyo
 
Da hapo laxima ujifanye mzimu tofauti na hapo inakula kwako
 
natoka vruuumhhh na pazia kama hamna basi nikuvaana na muombolezaji yeyote alieko mbele yangu nakumvua chochote mradi kuficha uchi wangu
 
kaka patamu hapo! itabidi uwe kama msukule tu hapo! ,lia kimaajabu huko chini ya uvungu wote watamkimbia marehemu basi fasts chukua nguo yoyote tokomea nayo ukabadilishe mbele ya safari ukaoge halafu urudi kwenye msiba uendelee kusikia gumzo lako...maana itakuwa ni ajabu kwa waombolezaji lazima wachomoke tu ndo nafasi yako...:flypig:
 
majibu mengine hutolewa kwenye tukio,jamani msifanye mchezo likutokee hilo.
 
kwel hivi ni vichekesho! loh, nimecheka kweli. natamani ingekuwa kweli, sijui ingempata nani! wanaume mna vituko!
 
hahahaaa! itabidi ujikaze kisabuni then unatoka kama hujui kitu vilee!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…