Vibweka uzunguni Joto City !!!

Bitoz

JF-Expert Member
Aug 27, 2015
30,823
126,549
Vipi makamanda laifu linasonga wanangu ? Last week nilipita uzunguni pande za Masaki na Oysterbay kupiga mishemishe kule...Basi nikanusanusa na kugundua vijimambo vyao ambavyo pia vipi sehemu za wenye vijisenti km kule Mikocheni n.k....

1/Vitoto vibwegebwege
Watoto wengi wa ushuani vimezidiwa maarifa na hata nguvu na watoto wa Uswaz...kwenye mihezo wanajua kucheza game tu na siku ukiweka mechi kati ya watoto wa kishua v wa Uswaz nahisi watapigwa bao za kutosha tu na kuibiwa vikorokoro vyao vyote .....Everything mabwegwbwege!!!

2/Toto kubwa linaogeshwa
Ukiingia kwenye mahekalu ya wenye nazo usishangae kumkuta beki tatu analiogesha na kulivalisha toto analolizidi miaka 5 tu...Toto linasoma standard faivu lakini halijui hata kuoga....full mdekezo !!!

3/Hawajui malavidavi
Mabinti na wavulana wa uzunguni hawajui sana mapenzi kulinganisha na watoto wa Uswahilini nahisi sababu wanafungiwa sana ndani hivyo. wanachelewa kujua mambo wakati uswahilini vitoto vidogo vinacheki"pilau" vibandani...wakikutana ni full mnyoosho !!

4/Mihogo Coco Beach
Pamoja na nyodo zao nimegundua Wateja wakubwa wa kutafuna mihogo ufukwe wa coco beach ni wakazi wa ushuani sisi watoto wa Uswahilini tunaenda beach wakati wa sikukuu ,wao hushinda kila siku...Hongereni !!!

5/Vinara wa vitambi na mandombolo
Wakazi wa uzunguni wanaongoza kwa matumbo makubwa na mawowowo wake kwa waume...sijui sababu kula kula sana au kutofanya mazoezi hadi kutofautisha demu na dume ni shughuli...full minyamanyama !!!

**** Jiachie...It's week end***

Sharobaro wa Uswaz
The Bitoz
 
wakati huku kwetu uswahilini tunacheza vigodoro na kutoboa vidirisha kuiba sub woofer na dvd...wao na washua wao wanajadili mikakati ya kuibia serikali millioni 20, na mbinu za kukwepa kodi..
 
wakati huku kwetu uswahilini tunacheza vigodoro na kutoboa vidirisha kuiba sub woofer na dvd...wao na washua wao wanajadili mikakati ya kuibia serikali millioni 20, na mbinu za kukwepa kodi..
Yaani wanakula bila jasho
Sisi full kutaabika
 
Back
Top Bottom