Vanila 1mil ni bei ya 2018. Vanilla iliyokauka.
Na ni bei ambayo haijawahi jirudia tena.
Ukiambiwa Vanilla Kagera ni 60,000/= basi zidisha kwa 10, unapata 600,000/=. Hiyo ndio inakuwa bei ya Vanilla iliyokaushwa.
Kwa ujumla Vanilla iliyokaushwa ni mara 10 ya bei ya Vanilla mbichi.
Njombe Vanilla haitokaa istawi itoe matokeo kama wanavyotaka Vanilla Village. Maana Vanilla haitaki baridi kali kama ya Njombe.
Watu wa Morogoro, Pwani, n.k wana fursa ya kulima Vanilla ya kutosha na sio Njombe.