Tetesi: Van Dabroek kutua Simba SC

James Hadley Chase

JF-Expert Member
Mar 25, 2020
1,587
2,677
Aliyewahi kuwa kocha wa Simba SC Sven Van Dabroek ambaye alifundisha FAR Rabat na Wydad Casablanca zote za nchini Morocco kisha akafundisha CR Belouzdad ya nchini Algeria anapewa nafasi kubwa ya kurithi mikoba ya Robertinho.

Kocha huyo kutoka Ubelgiji anatajwa kuwa chaguo la kwanza la uongozi wa juu wa Simba SC, na tayari ameanza mazungumzo ya awali, na kama mambo yatakwenda vizuri basi muda wowote kuanzia hivi sasa atatangazwa kuwa kocha mkuu klabuni hapo.

Kikosi cha Simba SC kinakwenda katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Namungo FC, ikiwa chini ya Kocha mzawa Seleman Matola pamoja na Kocha wa makipa Dan Cadena.

Simba SC itacheza mchezo huo keshokutwa Alhamis (Novemba 09), katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
 
Sawa
 
Akija na yeye akapigwa Tano anafungishwa virago na Wana msimbazi wakiongozwa na yule mpayukaji wataanza kuponda hafai hafai hafai kocha hatufai na vilio juu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…