Uzuri wa kitu upo machoni mwa mtu

Ze Rock

JF-Expert Member
Sep 15, 2020
270
563
Waiter mwambie Dj apunguze sauti ya mziki kidogo naongea na ma greater thinker....

Hi Jf members!

Leo bhana tulikuwa kama kaubishi flan hv katika kilinge chetu cha kujitafutia kipato.
Kama kawa akaja jamaa mmoja hv akaanza tu ghafla na story ya kuwa anamiliki Pisi moja kali kwa mujibu wa sifa alizozitoa nikasema au anamiliki jini nn?

Au Cleopatra karudi tena duniani? Manake alimwaga sifa aisee, Mara mtoto kiuno dondola, Jicho kama la ng'ombe , Guu la bia, umbo namba nane , Ngozi laini ka Sufi na kubwa zaidi mtoto ana hela kama zote! Mm nikapata wazo asije akawa anamzungumzia mke wa Jeff Benson nikamuomba atupnyeshe kapicha kidogo kuverify aliyoyasema yaani kabla sijamaliza mshkaji zamani katoa simu yake katoa password mara paap! Tunaonyeshwa mrembo na kusema mulifikiri uongo?

Cha ajabu kila mtu akawa anacheka na kusema bora wa kwangu demu gani huyo? Sema vumilia hela si umesema zipo? Nikaanza kumuona jamaa anaanza kuwa mpole gafla akatulia na kwa upole akauliza kwa hiyo siyo pisi kali? Watu wakamjibu ww unaonaje? Akasema Pisi kali tukamwambia ishi humo humo kwa kuwa uzuri wa kitu upo kwenye macho ya mtu.....

Na humu wapo pia kila mtu PISI KALI , PISI KALI ila ukali wanaousemea na sifa wanazozitoa haziendani kabisa na ukweli uliopo. Wachache wakweli wanasema kabisa pisi ya kawaida tu....

Ukijisifu sana na mapokeo yakawa si kama ulivyotegemea jikaze mtoto wa kiume!

Waiter Mwambie DJ aweke ile nyimbo ya Hidaya ya Pepe kale, njoo na Konyagi kubwa na ka energy

Karibuni Jf members
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom