asakuta same
JF-Expert Member
- Mar 1, 2011
- 14,829
- 5,039
Nchi za wenzetu kauli ya kiongozi inatosha kumfanya kiongozi awajibike kisiasa kwa kuachia wadhifa wake.
Tofauti na hapa Tanzania viongozi wamekuwa wanatoa maneno yenye utata , ubaguzi , kejeli , chuki , dharau na uongo bila kuzichukulia hizo kauli uzito wowote.
Leo hii anasimama waziri mkuu anasema " hizi fedha si za umma" , halafu imakuja kudhibitika ni za umma na umetumika udanganyifu kuzipora lakini hatuoni umuhimu wa yeye kuwajibika kwa kauli yake hii.
Leo hii anasimama waziri wa nishati na madini anadanganya ndani ya bunge kwa kejeli na ubabe na anasema fedha zilizodhibitika na mkaguzi mkuu wa Serikali ni fedha za Umma , lakini inaonekana hamna umuhimu wa yeye kuwajibika kwa kauli yake hii.
Leo anasimama katibu mkuu wa wizara anadanganya anapotosha na anakejeli mbunge , lakini tunaona hakuna umuhimu wa kumuwajibisha huyu kwa kauli yake.
Leo hii ana simama mwanasheria mkuu wa serikali anayekejeli kwa kumuita mbunge ndani ya bunge "tumbili" , "hizi fedha siyo za umma" , mimi ndiye niliidhinisha zitoke" , leo hii inaonekana hakuna umuhimu wa hawa watu kuwajibika.
Kama TAIFA la Tanzania ndiyo tupo hapa basi Viongozi wetu wa umma ni genge la wahuni kama wakaao vijiweni lisilojali linataamka nini , wapi na wakati gani.
Imefikia mahali tumechoka kuibiwa fedha zetu na watu tuliowakabidhi dhamana ya kutulindia , Watanzania tuchukue hatua sahihi kuiwajibisha hii serikali ya wezi na watetea wezi.