Uzi maalum kwa waliofumaniwa na kusutwa

stickvibration

JF-Expert Member
Feb 7, 2017
3,227
5,132
Habarini wakuu,

Kama mada inavojieleza hapo juu. Sioni sababu ya kusema mengi saana
Isipokuwa hakuna siku ambayo sintoisahau kama ile sikukuu ya VALENTINE DAY.

Nilimdanganya dem wangu kuwa nimepata safari ya ghafla ya kwenda Dar kikazi,
Huku nikawa nimeshampanga mchepuko wangu ntatoka nae Dinner usiku wa Valantine day.

Za mwizi ni 40, hiyo hoteli tulioenda na mchepuko wangu ndio kulikuwa kukifanyika Happy Birthday ya Dada yake na Dem wangu. Sikutegemea kama watafanyia Hapo hio sherehe yao kutokana na hio hotel ilikua ni nje kabisa ya mji.

Baada ya kufumaniwa la kwanza niliulizwa “ENHEE,!!!HAPA NDIO DAR”?

Hiyo siku nilichambwa sikubakizwa hata kidogo. Usiombe ukachambwa ama kusutwa na mwanamke wa kinyamwezi utatamani uzaliwe upya.

Huo ndio ulikua mkasa wangu ulionikuta.
 
Back
Top Bottom