Uzazi kwa njia ya operation (Ushauri) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uzazi kwa njia ya operation (Ushauri)

Discussion in 'JF Doctor' started by Mvaa Tai, Feb 6, 2012.

 1. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #1
  Feb 6, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Wakuu naomba ushauri, nina mtoto wa mwaka mmoja na miezi Miwili na mipango yetu ni kuwa na watoto wawili tuu Mungu akipenda, na tulipendelea wasipishane sana umri, ili tumalize mambo ya uzazi tuendelee na mambo ya ulezi na Shughuli nyingine. lakini kwa bahati nzuri au mbaya huyu first born wetu alipatikana kwa njia ya operation, je kiafya kwa umri huu wa mtoto yaani miezi 14 ni sahihi kwa mama yake kushika ujauzito mwingine???. Nishaurini kistaarabu ushauri wenu nitaufanyia maamuzi.
   
 2. I

  Ikunda JF-Expert Member

  #2
  Feb 6, 2012
  Joined: Jul 12, 2010
  Messages: 722
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kijana ni kwa nini msisubiri hata miaka miwili iishe??, huyo first born wenu anyonyi??
   
 3. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #3
  Feb 6, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Binafsi ningeshauri msubiri afikishe mi angalau miaka miwili ndio mtafute mwingine.

  Na kuhusu kuzaa kwa operation inategemea na kilichosababisha. . . kama ujauzito wake wa kwanza ulikua na complications amwone daktari kwa ushauri kabla ya kushika mwingine.
   
 4. Uda

  Uda JF-Expert Member

  #4
  Feb 6, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 730
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kwanza kwann alijifungua kwa operation?kwa utaalamu zaidi anatakiwa akae at least 4 two yrs,ili ile scar ya kwenye uterus i heel vzur,and to avoid other complication!
   
 5. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #5
  Feb 6, 2012
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  mukuu wangu! hapo kwenye red hujasomeka!
   
 6. Uda

  Uda JF-Expert Member

  #6
  Feb 6, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 730
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Namaanisha akae miaka miwili ndo abebe ujauzito mwingne!
   
 7. Uda

  Uda JF-Expert Member

  #7
  Feb 6, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 730
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Namaanisha akae miaka miwili ndyo abebe ujauzito mwingne!
   
 8. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #8
  Feb 6, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Ishu ni kwamba mtoto alikaa vibaya asingeweza kutoka kwa njia ya kawaida.
   
 9. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #9
  Feb 6, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Rejea post number 8
   
 10. doctorz

  doctorz JF-Expert Member

  #10
  Feb 6, 2012
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 907
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kuwa na subira. Miaka 4 kwa uterus scar ipone vizuri. Na kama mtoto alikaa vibaya, kwa nini hakuonekana mapema na kufanyiwa ECI? Ni hatari kupata mimba za juu kwa juu hasa kwa mwanamke alliye fanyiwa CS. Poleni sana na muwe na subira.
   
Loading...