Uzawa maana yake nini?

NDD:

Companero ana-limit upeo wake katika vitu viwili tu, uzawa na uraia. Labda tuongezee upeo wa mjadala huu kwa kuongeza maana. Kwa mfano:
- Kuna watu asilia (indigenous)
- Kuna wazawa (natives)
- Kuna raia (citizens)
- Kuna wazalendo (Patriots)
- Kuna wakazi wa kudumu (Permanent residents).

Watanzania mke na mume wanapopata mtoto wakiwa na uraia wa Marekani au UK, bado asili ya mtoto yule ni Tanzania.

Watanzania wenye asili ya kihindi waliozaliwa Tanzania, ni wazawa wa nchini Tanzania.

Uraia wa nchi unaweza kupatikana kwa sababu ya asilia, uzawa au kubadilisha.

Uzalendo ni mapenzi ya nchi ambayo yanaonyeshwa katika ulinzi wa interests za nchi.

Wakazi wa kudumu ni wahamiaji wenye uraia wa nchi nyingine.

Kama nimekosea naomba usahihisho wa maelezo yangu hili upeo wetu usiwe limited katika Uzawa na uraia wakati kuna vitu vingi.
 
Companero una-limit upeo wako katika vitu viwili tu, uzawa na uraia: Ngoja tupambanue zaidi:

- watu asilia (indigenous)

Tukirudi kwenye posti yako: kwenye utendaji wa kazi kuna kitu kinachoitwa ETHICS. Watanzania wengi hawana ETHICS katika utendaji wa kazi. Hivyo matatizo aliyopata Gavana sio matatizo ya kiuraia bali ya ethics kwa sababu waliomtangulia nao walifanya madudu hayohayo.
 
Companero una-limit upeo wako katika vitu viwili tu, uzawa na uraia: Ngoja tupambanue zaidi:

- watu asilia (indigenous)
- Kuna wazawa (natives)
- Kuna raia (citizens)
- Kuna wazalendo (Patriots)
- Kuna wakazi wa kudumu (Permanent residents).

Ewaa. Sasa tuko kwenye mstari mmoja. Na tuendelee. Taratibu. Hatua kwa hatua.

- Deutch Ostafrika (Tanganyika) ilianza kuwa nchi baada ya Kongamano la Berlin la 1884-1885. Wakati huo watu wote waliokuwa kwenye eneo lililo ndani ya Tanganyika hawakuwa wazawa wala watu wa asili ya Tanganyika.

- Tanzania ilianza kuwa nchi baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964. Wakati huo watu wote waliokuwa kwenye eneo lililo ndani ya Tanganyika hawakuwa wazawa wala watu wa asili ya Tanzania

Hitimisho: Kilicho muhimu ni uraia na uzalendo!
 
Last edited:
Compareno,
Mkuu naomba ufafanuzi ktk maneno haya (highlighted):-
- Deutch Ostafrika (Tanganyika) ilianza kuwa nchi baada ya Kongamano la Berlin la 1884-1885, Wakati huo watu wote waliokuwa kwenye eneo lililo ndani ya Tanganyika hawakuwa wazawa wala watu wa asili ya Tanganyika.
 
Mkuu namaanisha kabla ya hapo kulikuwa na falme, koo na tawala mbalimbali. Zingine zilikuwa zimeshawasili ndani ya eneo husika ambalo baadae lilikuja kuitwa Tanganyika na sasa linaitwa Tanzania Bara. Na zingine ndio zilikuwa zinawasili. Rejea historia ya makundi haya:

1. Wangoni - Waliingia eneo hili katika karne ya 19
2. Wamasai - Waliingia eneo hili katika milenia ya 1

Na, haya je: Wahaya? Wapare? Wasambaa? Wachagga? Wamakonde? N.K?

Tukimtafuta mzawa na muasilia halisi wa Tanzania, nani atasimama?

Naendelea kusisitiza: Mtanzania halisi ni Raia na Mzalendo wa Nchi hii!
 
Naomba usahihishe mwaka wa muungano huku tukiendelea.

Wewe si mlokole kama unavyodai mwenyewe. Kwa mantiki unayotumia taifa la wayahudi alitakiwi kuwepo.
 
Wewe si mlokole kama unavyodai mwenyewe. Kwa mantiki unayotumia taifa la wayahudi alitakiwi kuwepo.

Kuna 'Ulokole' wa aina nyingi. Wa kwangu unaamini kuwa leo Taifa la Wayahudi halipaswi kuwepo pale kwenye makazi ya Wapalestina. Ila lile Taifa la Wana wa Israeli wa Kale lilipaswa kuwepo kwenye Nchi hiyo ya Ahadi baada ya kulowea nyumbani kwetu Misri. Na hiyo Kanaani, Nchi ya Ahadi, si kwamba ilikuwa ni yao ya 'asili' au ya 'uzawa' bali Mungu aliamua tu kuwazawadia kutokana na imani na utii wa Babu yao Ibrahimu/Abrahamu na mwanawe Isaka pamoja na Baba yao Yakobo/Israeli. Baada ya kuasi, Mungu akawasambaza duniani. Sasa Utaifa wa Israeli ni suala la Kiroho.

Asante kwa kuleta hili suala ya Wayahudi. Linasaidia sana kuonesha jinsi gani dhana ya 'uzawa' ilivyo tata na tete hasa katika dunia/ulimwengu huu uliochangamana sana. Utumwa, Ukoloni, Ubeberu na Utandawazi vimetufanya tusambae na tuchanganyike sana. Hivyo, dhana ya 'uraia' ikitungiwa sera na sheria nzuri ndio inaweza kutusaidia kuishi kwa pamoja vizuri bila migongano mizito ya 'wazawa' dhidi ya 'walowezi', 'waasili' dhidi ya 'wageni' au 'raia' dhidi ya 'wakimbizi'. Sheria hiyo inapaswa kuhakikisha uraia = uzalendo na ichukue mkondo wake ikitokea mnaufanya uraia = ufisadi.
 
Kwa mtaji huu, unakubaliana nami kuwa sheria za sasa sio nzuri. Kwa mfano zinamnyima haki mtanzania kuwa na uraia wa nchi mbili na mambo mengine.
 
Kwa mtaji huu, unakubaliana nami kuwa sheria za sasa sio nzuri. Kwa mfano zinamnyima haki mtanzania kuwa na uraia wa nchi mbili na mambo mengine.

Nakubaliana nawe kwenye sentensi ya kwanza hapo juu. Mifano yangu kuhusu hilo unaijua, ipo kwenye ile mada. Huo mfano wako hautambuliki hata kwenye Tamko la Dunia la Haki za Binadamu (Universal Declaration of Human Rights). Hiyo unayotaka siyo haki (right). Ni fadhila (privilege). Hatukupi. Ng'o!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…