Sawa ni uzalendo wa kweli ila wanatakiwa waende mbele zaidi, kwa kujitolea michango yakifedha ili timu ijitegemee kwani cha ajabu Mbeya city bado wanakula kwa mama lishe!!!!! Kama mashabiki wao wanaweza kukodi magari kumi hadi dar inakuwaje washindwe kuichangia timu? Haya ndio matatizo yanayozikumba timu zetu mwanachama anashindwa kuchangia sh.elfu 15 kama ada ya uanachama kwa mwaka!!! Ila anaposikia kuna watu wanataka kuingia mkataba na timu anapiga kelele kuwa ni pesa ndogo!! MBEYA CITY wekeni mambo sawa nyie na azamu ndio tegemeo jipya la mpira wa tz achaneni ni hizi timu kongwe ambazo hata viwanja vyao tu vimewashinda kujenga!