Unaweza kuuliza mambo ya maisha yake ambayo yana maana tu kwa wakati huo na hata kwa baadae, kuna maswali mengine kuulizana ni kuchoshana tu, na ujue kuna watu hawapendi maswali yasiyo na tija.
Mf; Umenikuta nina kazi yangu nzuri tu, labda ukaniuliza nilihitimu chuo gani hiyo fani ninayofanyia kazi, hili swali siyo baya mi nakujibu tu shoti UDSM. Sasa kimbembe kinakuja unaongeza maswali, eti ukuwahi kurudia darasa? ulipitia qt? 4m 1 umesoma mara ngapi, Umerisiti 4m 4 mara ngapi? Nianze kukuelezea historia du! Akipenda kukwambia mwache aeleze mwenyewe asipopenda kausha