UVCCM acheni siasa za majitaka

mwembemdogo

JF-Expert Member
Feb 28, 2016
2,282
1,252
Napenda kuchukua nafasi hii kuuambia uongozi wa UVCCM uache kuendesha siasa za Maji taka.Hivi karibuni umoja huo umekuwa unatoa matamko yasiyo Na mashiko wa Tija Kwa CCM.

Umoja huo umekuwa hautaki mtanzania yoyote asitoe maoni take Juu ya serikali Na viongozi wake.

Umoja huo unapaswa kujua kuwa hii nchi ni ya watanzania wote Kwa mujibu wa katiba Yetu kila RAIA ana haki ya kutoa mawazo yake.

Mh. Sumaye Waziri MKUU mstaafu ametoa mawazo yake Juu ya Mh.Rais lakini UVCCM wamemjia Juu utadhani moto wa kifuu.

UVCCM in lazima wawe Na heshima Na adabu kwani viongozi wastaafu kama Waziri MKUU wana haki kikatiba kusema ili mradi hawavunji Sheria.Kosa la Mh. Sumaye ni nini?

Rais sio wa wanaccm ni wa watanzania wote amepigiwa kura Na wasio wanaccm Na nijukumu letu kumkosoa kumshauri kumwomba ili mradi sio kumtukana.

Tunaushauri UVCCM iwaheshimu viongozi walioliongoza Taifa hili Na ndio maana mpaka Leo hii serikali inawatambua na kuwalipa stahili zao UVCCM acheni kuwadharau Viongozi Wastaafu.
 
Naona malipo yameongezeka UFIPA maana kila dakika naona mabandiko tu kuhusu ccm na Serikali kwa Ujumla.

lakini kukusaidia tu kwa kile kilichosemwa na MZEE SUMAYE nadhani aliegemea mlengo na hulka ya chama chake katika kupinga hata kile ambacho ni sahihi.

hakatazwi mtu kutoa maoni lakini mnapoona mtoa maoni anapotoka kwa kuongea uongo! Hakuna njia nyingine ya kufanya Zaidi ya Kuweka sawa kile kilichopotoshwa
 
Back
Top Bottom