Utumishi wa Umma: Uhakiki wa Mishahara Hewa Waanza

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
mag2.jpg

Siku chache baada ya wakuu wa mikoa kuapishwa na Rais John Magufuli, imeelezwa kuwa wakuu hao wametoa agizo la kuhakiki taarifa za watumishi wa umma kwenye mikoa yao.

Agizo hilo la Rais linalenga kubaini watumishi hewa katika mikoa na wilaya nchini. Kazi hiyo imeanza kutekelezwa kwenye baadhi ya hospitali za Serikali nchini.

Taarifa zilizoptaikana jana, zimeleza kuwa Hospitali ya Wilaya ya Temeke na nyingine za mikoani, watumishi wote wametakiwa kupeleka viambatanisho kadhaa kwa ajili ya uhakiki wa taarifa zao za ajira.

Chanzo kutoka hospitali ya Temeke kilieleza kuwa viambatanishi hivyo ni pamoja na barua ya ajira, wasifu wa kazi na stakabadhi ya malipo ya mshahara.

Chanzo hicho kilisema kuwa agizo hilo lilitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na wafanyakazi wanatakiwa kukabidhi viambatanisho hivyo kuanzia wiki hii.

Ofisa Uhusiano wa Manispaa ya Temeke, Joyce Msumba alisema,“Hatuhakiki watumishi wa sekta ya afya tu ni watumishi wote wa umma.”

Alisema watumishi ambao wako nje ya vituo vyao vya kazi, wametakiwa kurejea mara moja kwa ajili ya kazi hiyo.
 
Nchi kwa kukurupuka haijambo. Hivi RC ndani ya siku kumi unampa jukumu la kubaini watumishi hewa kwa halmashauri zote za mkoa wake sii kutegemea taarifa za uongo tuu?
Kwa nini zisitumike Ofisi za Ma DSO zisitumike?
 
mag2.jpg

Siku chache baada ya wakuu wa mikoa kuapishwa na Rais John Magufuli, imeelezwa kuwa wakuu hao wametoa agizo la kuhakiki taarifa za watumishi wa umma kwenye mikoa yao.

Agizo hilo la Rais linalenga kubaini watumishi hewa katika mikoa na wilaya nchini. Kazi hiyo imeanza kutekelezwa kwenye baadhi ya hospitali za Serikali nchini.

Taarifa zilizoptaikana jana, zimeleza kuwa Hospitali ya Wilaya ya Temeke na nyingine za mikoani, watumishi wote wametakiwa kupeleka viambatanisho kadhaa kwa ajili ya uhakiki wa taarifa zao za ajira.

Chanzo kutoka hospitali ya Temeke kilieleza kuwa viambatanishi hivyo ni pamoja na barua ya ajira, wasifu wa kazi na stakabadhi ya malipo ya mshahara.

Chanzo hicho kilisema kuwa agizo hilo lilitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na wafanyakazi wanatakiwa kukabidhi viambatanisho hivyo kuanzia wiki hii.

Ofisa Uhusiano wa Manispaa ya Temeke, Joyce Msumba alisema,“Hatuhakiki watumishi wa sekta ya afya tu ni watumishi wote wa umma.”

Alisema watumishi ambao wako nje ya vituo vyao vya kazi, wametakiwa kurejea mara moja kwa ajili ya kazi hiyo.

Waajiri hawana taarifa za watu wao? hadi wajiriwa ndio wajithibitishe? lahaula....
 
Swala la watumishi hewa ni ngumu sana kulimaliza coz wapo wanaokufa wapo wanaocha kazi bila hata ya kutoa taarifa wapo wanao staafu yupo rafiki yangu ameacha kazi ana mwaka na nusu lakini mshahara unaingia kama kawa japo boc wetu alipeleka taarifa zake kwa maafisa utumishi lakini cha ajabu akuna kilicho fanyiwa kazi tatizo ni umakini tu haupo katika idara ya afisa utumishi
 
Tatizo linatoka Utumishi ni wazembe Na mfumo wao
 
DAWA ni RC,MKURUGENZI,AFISA UTUMISHI NA RAS kupita wao wenyewe shule kwa shule,hosoital kwa hospital na ofisi kwa ofisi apo watabaini madudu mengi lakini hii ya ujumlajumla ni kuendeleza zimwi lilelile maana wafanyakazi hewa ni wengi hasa idara ya elimu watu walieenda kusoma miaka na miaka lakini kwenye payrall wapo na walishaacha kazi...watu walishakufa ila salary slip zao zinatoka mpaka kesho..HIvyo serikali km haitahakiki kituo kwa kituo ni kijidanganya tu...
 
Wapeleke na vyeti vya TAALUMA ili kuepusha wauguzaaaaa Feki, kuepusha kuto panda vyeo na mishahara kwa watumishi wengi nchini, kuepusha upendeleo, na mengi mengineyo, serikali isiangalie hasara ya wafanyakazi hewa , iangalie ni wafanyakazi wangapi pia hawapati stahiki zao ku lingana na either elimu zao au muda walio tumikia sekta mbali mbali ( kuanzia serikali kuu hadi serikali za mitaa) kwa kufanya hivi nadhani itakua ni WIN WIN situation
 
Kuna jambo ambalo hapa linaleta maswali.Ni kweli zoezi la uhakiki ni zuri ila ningetaka nijue hivi utumishi/halmashauri wana database ya watumishi ambayo iko updated .manake hata tukifanya uhakiki alafu hatuna "mifumo"mizuri ya kutunza taarifa baada ya muda flani kuna wahuni wata-temper na majina ya watumishi.

Mfano:
Juzi hapa nimeona maafisa habari wakisisitizwa kutoa taarifa kwa uma zinapohitajika,ila ikumbukwe kuwa karibu idara na taasisi zote za serikali zina website ambazo nyingi haziko up to date au ukitumia contacts zao kuwasiliana kama email umeumia! hadi uende physically.

Nadhani imefika wakati tuwe makini tunapohakiki.tuboreshe database ili zitumike ipaswavyo isiwe ikawa kila siku ni "back to square one".

Na wale wanaohusika na hizi"blunder" wanachukuliwa hatua gani?
....haki ionekane imetendeka..
 
Mhhhh! hili zoezi kila mara linafanyika lakini watumishi hewa hawaishi! Labda safari hii itakuwa tofauti. Tusubiri tuone!
 
Swala la watumishi hewa ni ngumu sana kulimaliza coz wapo wanaokufa wapo wanaocha kazi bila hata ya kutoa taarifa wapo wanao staafu yupo rafiki yangu ameacha kazi ana mwaka na nusu lakini mshahara unaingia kama kawa japo boc wetu alipeleka taarifa zake kwa maafisa utumishi lakini cha ajabu akuna kilicho fanyiwa kazi tatizo ni umakini tu haupo katika idara ya afisa utumishi

Hawa maafisa utumishi sijui kwanini wako hivi kila sehemu......wanahutaji reform pengine kwenye mafunzo yao au labda kuna kamfumo ambako hakako rasmi wamekaanzisha baina yao. Kwenye sehemu yangu ya kazi kuna inconsistency ya ajabu kwenye taarifa za waajiriwa. Na wamekosa umakini hata katika mawasiliano.
 
Nd
Kuna jambo ambalo hapa linaleta maswali.Ni kweli zoezi la uhakiki ni zuri ila ningetaka nijue hivi utumishi/halmashauri wana database ya watumishi ambayo iko updated .manake hata tukifanya uhakiki alafu hatuna "mifumo"mizuri ya kutunza taarifa baada ya muda flani kuna wahuni wata-temper na majina ya watumishi.

Mfano:
Juzi hapa nimeona maafisa habari wakisisitizwa kutoa taarifa kwa uma zinapohitajika,ila ikumbukwe kuwa karibu idara na taasisi zote za serikali zina website ambazo nyingi haziko up to date au ukitumia contacts zao kuwasiliana kama email umeumia! hadi uende physically.

Nadhani imefika wakati tuwe makini tunapohakiki.tuboreshe database ili zitumike ipaswavyo isiwe ikawa kila siku ni "back to square one".

Na wale wanaohusika na hizi"blunder" wanachukuliwa hatua gani?
....haki ionekane imetendeka..

Ndugu yangu hii nchi katika halmashauri karubu zote tatizo ni hakuna data base. Nimekuwa nikijiuliza hawa huwa wanapangaje maendeleo yao bila kuwa na profile ya wilaya ama halmashauri?

Amini usiamini watendaji wa vijiji wana profile nzuri kuliko hao waliopo halmashauri ya wilaya.

We jarubu kwenda kwenye halmashauri zetu alafu uliza keenye halmadhauri zao wafanyabiasha wapo wangapi, wafanyakazi wa umma wapo wangapi walioahiriwa sector binafsi ni wangapi; mifugo ipo kiasi gani; ardhi ipo kiasi gani na aina zipi duu...jibu utalipata kiwa kaulize ofisi fulani...uncoordinated kama hizo ofisi zinataarifa kwanini kusiwe na one stopping shop yenye taarifa zote? Kama hizi taarifa hazijulikani wanawekaje mipango ya maendeleo?
 
Kwan mwenye mamlaka ya kujua,wafanyakaz wangap wamestaaf,wameacha kaz,wamefukuzwa,wameenda shule,wamefungwa jela ni nan?
 
Nd

Ndugu yangu hii nchi katika halmashauri karubu zote tatizo ni hakuna data base. Nimekuwa nikijiuliza hawa huwa wanapangaje maendeleo yao bila kuwa na profile ya wilaya ama halmashauri?

Amini usiamini watendaji wa vijiji wana profile nzuri kuliko hao waliopo halmashauri ya wilaya.

We jarubu kwenda kwenye halmashauri zetu alafu uliza keenye halmadhauri zao wafanyabiasha wapo wangapi, wafanyakazi wa umma wapo wangapi walioahiriwa sector binafsi ni wangapi; mifugo ipo kiasi gani; ardhi ipo kiasi gani na aina zipi duu...jibu utalipata kiwa kaulize ofisi fulani...uncoordinated kama hizo ofisi zinataarifa kwanini kusiwe na one stopping shop yenye taarifa zote? Kama hizi taarifa hazijulikani wanawekaje mipango ya maendeleo?
Kama ndo iko hivyo...
tuendelee kutatua tatizo bila kufanyia kazi mzizi wa tatizo!
 
Mm naamin wao ndo wanazo data sahii kuhusu wafanyakaz wao,maana kumbukumbu wanazo
 
Back
Top Bottom