Utumishi/Hazina: Watumishi wa serikali walishwa mkono mtupu sikukuu ya Krismas na mwaka mpya

hp4510

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
7,000
7,156
Watumishi kadhaa, wengi wao wakiwa ni waalimu wa shule za sekondari nchini hawataiona/ wala kuonja tamu ya X-Mass wala mwaka mpya kwa kuwa maafisa utumishi kwenye halmashauri zao walizembea ku update taarifa zao za historia na kupelekea kufutwa katika payroll hazina kuu. Katika hao wapo pia wengine katika idara za kilimo, ujenzi, ardhi, n.k.

Wenginee ni wahudumu kutoka afya. Baadhi yao, walishajaza sana taarifa binafsi lakini uzembe umeonekana katika maafisa utumishi, kuwasababishia mateso watumishi wengi katika sekta ya umma, kukosa raha na kununua mahitaji ya sikukuu kubwa kabisa ya X-mass na mwaka mpya..

USHAURI: HAZINA IHAKIKISHE INAWAPATIA HARAKA FEDHA ZAO ili wajiunge na umma duniani katika sherehe hizi muhimu.
 
Wengi wao ni miungu watu, na kwabahati mbaya zaidi akiwa na vimiwani basi ni shida, anakutazama kama nyanya mbichi

Kweli mkuu!!!,hayo yamenikuta majuzi nilipokuwa ninafuatilia Upandishwaji wa Madaraja,yaani jamaa anavyoniangalia ni kama nimejipaka kinyesi,looh!!,hawa jamaa wanajiona kweli kweli.
 
Kweli mkuu!!!,hayo yamenikuta majuzi nilipokuwa ninafuatilia Upandishwaji wa Madaraja,yaani jamaa anavyoniangalia ni kama nimejipaka kinyesi,looh!!,hawa jamaa wanajiona kweli kweli.

Dawa yao ni kusubiri waziri Mkuu au Rais mwenyewe amekuja wilayani kwenu unatupia swali kwenye mkutano umwone atakavyojikojolea! Kwenye ugeni huwa wananywea wanakua wadogo kama punje ya haradali!
 
Afisa utumishi tabora manispaa ni mzigo sijawahi ona duniani hapa,walimu wamepandishwa daraja 30/6/2015 mpaka leo mishahara haijabadilika,natamani sana ziara ya waziri husika tabora.yaani ni shida kubwa saaaannaaaaaa
 
Dawa yao ni kusubiri waziri Mkuu au Rais mwenyewe amekuja wilayani kwenu unatupia swali kwenye mkutano umwone atakavyojikojolea! Kwenye ugeni huwa wananywea wanakua wadogo kama punje ya haradali!
Yaani mkuu bora Mh.Rais na Waziri Mkuu waanze kukutana na Watumishi kwenye Halmashauri na Idara za Serikali kusikiliza kero za Watumishi hakika watayasikia mengi,hapo walau tutachapa kazi kwa moyo mweupe bila kinyongo.
 
Back
Top Bottom