everlenk
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 11,628
- 15,027
Heri ya mwaka Mpya wana MMU, natumai wote ni wazima kwa kudra za mwenyezi Mungu tumeona tena Mwaka.
Leo ningependa tujikumbushe jambo dogo sana katika maisha Yetu tuwapo hapa duniani hasa katika mahusiano yetu yoyote Yale ya kindugu,kirafiki ama kimapenz. Tunajua Mungu hakutuumba sisi sote tukiwa kamili kila mtu ana udhaifu wake na ukamilifu wake, hivyo basi tofauti zipo katika maisha.
Kwakuwa tofauti zipo basi ni wajibu wetu kuzichukulia tofauti hizo katika mlengo wenye kuleta tija(take it in a positive way) huku ukimsaidia mwenzako huyo kutoka katika udhaifu/ mapungufu hayo taratibu lakini isiwe ndo fimbo ya kumchapia katika upungufu ule alio nao.
Mfano Kama hapa duniani kila mtu angelikuwa ni tajiri,amejikamilisha kwa kila kitu ni dhahiri kusingekuwa na mtu anayemuhitaji mwenzake,tupo madaraja mbalimbali na kila Mmoja ni faida kwa mwenzake, je ingelikuwa vipi kama huu ulimwengu ungekuwa ni wa wanaume tu au wanawake tu hakika ungeboa sana. Huu ulimwengu ungekuwa na wasomi tu vile vile ungekuwa mbaya maana hawa wasomi wangepata wapi study zao?
Pengine mpenzi wako anaweza kuwa muongeaji sana kiasi kwamba ni kero kwako,isiwe sababu ya kumtenda na kugombana kila siku au kumuona yeye hafai, kwanza ukubali kwamba huo ndo udhaifu wake,msaidie naye kujielewa huku ukimuelimisha kwa utaratibu namna gani huo uongeaji wake anaweza kuutumia kwa ustaarabu pasipo kuwa kero Kwenu kisha namna gani hicho kipawa cha uongeaji anavyoweza kukitumia vizuri, pengine anaweza kuwa MC mmoja mzuri sana na akaongeza pato la familia au akawa msaada hata kwako kupenya sehemu zile ambazo wewe usiye muongeaji usingeweza kufika. Yaani ni kama vile unatumia fursa lakini yenye kujenga na si kubomoa.
Madhaifu yetu yanatufanya sisi tuwe kamili,huyu ana moja mwingine ana mbili tukizijumlisha ni tatu, pengine unaweza kuwa mzuri sana kwenye kutafuta lakini si mzuri wa kuhifadhi,pengine ni mzuri sana wa kupanga lakini si mtekelezaji,pengine una yote ya muhimu ila umekosa wa kukufanya ufurahi ,kila mmoja ni wa faida kwa mwenzake na ana vitu unique ambavyo mwenzake hana ni kuheshimiana na kujaliana tu, mwanaume anamuhitaji mwanamke kuwa kamili vile vile mwanamke anahitaji mwanaume kuwa kamili, Tupendane na kuheshimiana sote ni wa muhimu kwa kila mmoja. Na Mungu atusaidie.
Nawatakia kila la heri kwa mwaka wa 2016 ukawe mwaka wa Neema katika maisha yetu ya kimahusiano.
Karibuni wote kwa nyongeza zaidi.