Uteuzi wa Kitila Mkumbo ni wa kimkakati!

JERUSALEMU

JF-Expert Member
Sep 19, 2012
3,112
3,536
Salamu wanajamvi !
Naam, ni kama amefanikiwa kimalengo baada ya kutulia na kuona namna gani jinsi ya kurudisha heshima yake ya kisiasa iliyo poromoka kwa kasi ya ajabu .Magufuli alikuwa hana chaguo jingine isipokuwa kunywa dawa chungu ili apone.Anajua kuwa umaarufu wake umeshuka sana ndani ya chama chake na nje ya chama chake.Umaarufu wake umeshuka mara dufu nje ya mipaka ya Tanzania kuliko tunavyo fikiri. Hakuna anaye mjadili Magufuli kwa zuri lolote! Hapo Kenya kwenye mjadala mmoja wamemwita ni Trump wa Afrika.Amemteua Kitila Mkumbo kimkakati na siyo kwa lengo la kuunganisha Nchi.sababu? Nitazieleza.

Kwanza naomba ieleweke kwamba Magufuli hana mapenzi thabiti na Nchi hii. Mwenye mapenzi na Nchi yake hawezi kutamani kuifuta TLS tu kwasababu Tundu Lissu amechaguliwa kuongoza chombo hicho.Tundu Lissu ana uwezo wa kuingoza TLS kwa mafanikio makubwa. Lakini Serikali ya Magufuli kwa kuwa hawaitakii mema Nchi wakatangaiza kutokuwapa ushirikiano TLS.

Pili, naomba ieleweke kuwa Magufuli huwapenda wapinzani pale tu anapo taka kuwatumia ili afikie Malengo yake kisiasa. Anamhitaji Lipumbavu ili aiangamize CUF.akifanikiwa ataachana naye! Kwa dhati ya moyo wake anatamani Nchi hii isiwe na mpinzani hata mmoja WalaKatiba, vinamkwaza kufika anako taka kwenda.A one man rule!

Kumteuwa Kitila Mkumbo kisiasa kumemnyanyua Magufuli kiasi. Wasio mjua vizuri wanadhani lengo lake ni kuunganisha Nchi. Wanakosea. Lengo lake Ni divide and rule! Anamhitaji sana Zitto Kabwe sasa kuliko wakati mwingine.Ana wakati mgumu Bungeni kwa mambo mawili. Moja ni bajeti zake zisizotekelezeka na pili ni kuhusu Mtoto mpendwa Bashite.ACT wakiwa upande wake anahisi atakuwa salama kiasi.Na kwa mbali naanza kuona amefanikiwa.Zitto hawezi kumsakama kwa kutoa hoja motomoto bungeni.Amemtuliza.

Magufuli amemteua Kitila Mkumbo ili Dunia Ione Ni Rais pekee Afrika ambae anafanyakazi na upinzani! Kumbe ni mkakati wake wa kujijenga upya kisiasa huko duniani.Kimsingi haaminiki tens kisiasa na kiuchumi.

Ndani ya nchi Magufuli amejiharibia nyota yake kwa mambo kadhaa. Mosi ni Sera sake za kiuchumi mbovu zimepelekea mambo mengi kusimama au kwenda kombo.wananchi wana maisha magumu sasa kuliko wakati wowote tangu Mwaka 1985! Lakini kumbeba Makonda kumemfanya aonekane ni mtu anae jali ukabila na kufahamiana! Magufuli Ni mbinafsi namba moja na hii imemfanya achukiwe hata ndani ya chama chake.Hapendi watu wapate fedha, anatamani wawe nasikini ili wamnyenyekee. Kumteua Kitila Mkumbo ni mkakati wa kutafuta uungwaji mkono nje ya chama chake ili wanaomsifia waongezeke. Na kwa hakika amempata Zitto Kabwe!!
 
JE ANGETEULIWA MREMA KUWA WA CHADEMA KUWA KATIBU MKUU ..TUNGESEMAJE??
 
Analysis nzuri. Niongeze tu kuwa huo ni mkakati maalum wa kumnyamazisha Zitto. Dalili zilikuwa zinaonyesha kuwa Zitto ankaribia kujiunga na Ukawa na kwa kweli Zitto amekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya Magufuli. Sasa kwisha habari yake, atasema nini wakati mshauri wake mkuu ameshajiunga na CCM?
 
Maneno mengi halafu ubwabwa mtupu tulieni dawa iingie kwanza ndiyo kwanza sindano inaingia hata dawa haijasukumwa
 
Ni kweli mkuu, hapa jamaa amefanikiwa kununua akili za Zitto. Maana baada ya uteuzi wa Kitila, Zitto ametokwa povu la haja kumsifia Magu kwamba eti ameamua kuunganisha nchi na ameona kuna watu bora ktk vyama vya upinzani. Soon tutaona rangi dhahiri ya Zitto.

Magufuli sasa anakaribia kufanikiwa kudhoofisha upinzani. Maana kwa Tanzania bara cuf naona ni kama imekufa, akizima na sauti za akina Zitto. Upinzani utabakia Chadema tu. Nako ikitokea akapandikiza mdudu wa fitina basi 2020 Magu hana wa kumhofia.
 
Wewe humfahamu Zitto Kabwe vizuri,atakunyenyekea pale anapohitaji kitu,akishakipata atakusumbua mno ili kurudisha heshima yake.Atakutumia na utamtumia pale anapokuwa na maslahi na wewe.Kama ccm itamhakikishia chama chake kukua basi yupo tayali kuwaangamiza wapinzani wote abaki yeye peke yake.

Kama pia akiona upinzani wenzake watamsaidia kukua kisiasa basi ataungana nao kwa hali na mali .Na usishangae 2020 akiungwa mkono na ccm na Cuf ya Lipumba ili apunguze kura kwa upinzani na hasa kula za dini ile atazipita vya kutosha.

Nachowashauri upinzani watafute platform moja ya kunadi sera zao.Waunde chama kimoja na waache uroho wamatumbo yao iIi wawe na nguvu moja.Haiwezekani upinzani wanachukuliana wanachama kama ilivyotokea ukawa(chadema) kwa kumchukua Kafulila na kufikiri iliwafurahisha Nccr Mageuzi(Mbatia).Kwahiyo upinzani wawe makini hasa chadema nakila hatua wanazopiga.

Nahio ndio sasa kukubali kutumika pale nawewe unaponufaika maana siasa za Tz bila unafiki hazinogi.Ndio maana chadema walikubali kumtumia Lowasa ili waende ikulu,na JPM anawatumia cuf(profesa)ili ajiimalishe kisiasa.Ni unafiki tu na kama huwezi unafiki siasa za Tz sio rafiki kwako.unahitaji kuwa mnafiki kama Nape,Lowasa,Zitto,Mbowe,Magufuli,Mbatia,Lipumba,Lisu ili ule matunda ya nchi yako tamu Tz.
 
Blaa blaa mingi sana nchi hii. Japo najua uteuzi wake ni maandalizi ya kumrudisha na kumpa cheo Dr. Slaa. Sitashangaa sana nikiona hata zito kateuliwa kuwa naibu waziri.

Anyway: Uteuzi huu ni funika kombe tu kwa ujio wa Slaa ndani ya serikali, kwa hiyo Kitila asishangilie sana.
 
Maneno mengi halafu ubwabwa mtupu tulieni dawa iingie kwanza ndiyo kwanza sindano inaingia hata dawa haijasukumwa
Mimi naona dawa anainywa Magufuli kwasababu analazimika kuyakubali matapishi yake mwenyewe.

Leo hii amemsamehe Ney wa mitego sio kwa kupenda! Alihofia kuendelea kuwapoteza wasanii Wengi zaidi baada ya Wema kumkimbia.

Amelazimika kumteua Kitila Mkumbo ili arudishe sifa yake kisiasa kwani alipoteza uungwaji mkono kwa kiasi kikubwa.
 
Back
Top Bottom