UTEUZI: Rais Magufuli amemteua Prof. Wangwe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya NSSF

Queen V

JF-Expert Member
Jan 19, 2012
775
1,332
DSC_6829.JPG


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amemteua Prof. Samwel Mwita Wangwe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuanzia tarehe tarehe 30 Mei, 2016 kwa kipindi cha miaka mitatu.

Uteuzi huo umefanyika kwa mujibu wa Sheria ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ya mwaka 1977 pamoja na marekebisho yake katika Sheria ya Msimamizi na Mdhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Na.5/2012. (The Social Security Laws (Amendements) Act.2012 jedwali la pili (Second Schedule) kifungu cha 2 (1).

Aidha, kwa mujibu wa Sheria hiyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista J. Mhagama amewateua Bw. Paul Daud Sangize – Mwakilishi wa Wafanyakazi, Bw. Noel Nchimbi – Mwakilishi wa Wafanyakazi, Bw. David Magese – Mwakilishi wa Waajiri kuwa Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Shirika la Taifa la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Wengine ni Bibi Margreth Chacha – Mwakilishi wa Waajiri, Bw. Justine Mwandu – Mwakilishi wa Sekta Binafsi, Bw. Gabriel Pascal Malata – Mwakilishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. Emmanuel Maduhu Subi – Mwakilishi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Ally Ahmed Msaki – Mwakilishi wa Ofisi ya Waziri Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu)
 
Nani katolewa kwenye hiyo nafsi? Nani alikuwa mwenyekiti wa hiyo bodi? Je alikuwa anastahili kubaki?
 
Hivi yule mwanafunzi wa UD anayekabiliwa na kesi ya 'mtandao' ni mtoto wa huyu Prof?
 
Ww soma tu, kama huna shule utasubiri saaaanaaa!!
Elimu yangu drs la 7,sitegemei siyo tu kuajiliwa au kuteuliwa na serikali bali hata mtu binafsi hawezi kuniajili ndio maana nimerizika na biashara yangu ya kuuza mkaa lakini nataka haki itendeke.
 
Elimu yangu drs la 7,sitegemei siyo tu kuajiliwa au kuteuliwa na serikali bali hata mtu binafsi hawezi kuniajili ndio maana nimerizika na biashara yangu ya kuuza mkaa lakini nataka haki itendeke.
Tulia sasa!! Hawana shule wenzio hao.
 
Kuna mwengine katupia kaudini na hapa kaukanda#kumbe urais kazi sana#

Mkuu wengine wanatupia kaujinsia hapa na pale.Hawaelewi dunia imebadilika unaangaliwa uwezo tu.Ujerumani raisi ni mwanamke Angela Merkel baraza lake la mawaziri lina mawaziri 15.Mawaziri wanawake ni watano tu waliobaki wote ni wanaume.
 
Back
Top Bottom