Lowasa na Sumaye ni watu wawili tofauti kabisaaaaaaaa
Sumaye
Katika maamuzi sio mkurupukaji, habari za ndani zinasema aliweza kufuatilia shughuli za serikali mpaka ngazi za wilaya kwa kuwaita na kuwakanya watendaji wabovu na wakajirekebisha kimyakimya, aliweza kusimamia ukusanyaji wa mapato ya nchi na uchumi ukawa unaimalika, kipindi chake madaraja, barabara hata hiyo sera ya shule za kata ilianza. Hakuutafuta uwaziri mkuu kivile kama EL alivyofanya mpaka wakapelekea sakata la EPA, hivyo hakuwa na deni la kulipa kwa wafanyabiashara na wadhamini mbalimbali kama EL, wafanyakazi na wafanyabiashara walikuwa wanaheshimiana sana kutokana na kurejesha heshima kwa wafanyakazi. Tusisahau, uwanja wa taifa......
Hata hivyo alikuwa na mapungufu yake kama vile kujilimbikizia mali, kushindwa kumshauri Ben juu ya ununuzi wa rada, ndege ya rais, kufanya biashara wakiwa ikulu, nyumba za serikali...
Lowasa
Mkurupukaji kwenye maamuzi, hakuweza kusimamia utendaji vizuri bali kutishia tu kupitia vyombo vya habari,au mikutano yao. Hakuwa na mbinu mbadala za kukusanya fedha/mapato bali kutumia tu walizoacha wenzao, bajeti zao za mwaka zilikuwa changa la macho hazitekelezeki tofauti na kipindi cha Sumaye.... Kashfa kubwa kubwa kama za EPA, Richmond na nyinginezo. Alitafuta uwaziri kwa nguvu zote hivyo alikuwa na wakuwalipa akiwa madarakani.... Hata hivyo alijitahidi kama ilivyosemwa hapo juu japo barabara 3 kwa hela walizokusanya wenzao...
Hitimisho.
Kwa kipindi kijacho hawa hawatufai maana hawana jipya....na sera za chama cha wakujikuna zimeoza hazitekelezeki...hasa huyu EL mzee wa misumu na kukurupuka. Nadhani, Chadema kwa kasi waliyonayo wanaweza kurekebisha hayo yote hapo juu.