Utekelezaji wa hukumu

Masanjaone

JF-Expert Member
Nov 15, 2019
844
596
Naomba kuuliza wanasheria, nilishinda kesi Mahakama Kuu, mdaiwa akapeleka Notice of Appeal Mahakama ya Rufaa na akakaa kimya japo hata notice hiyo hakunisevu.

Muda wa rufaa ulipoisha nikaenda kukaza hukumu, msajili akaweka pending maombi yangu ya kukaza hukumu, kwa kigezo cha Notice of Appeal japo sikuwa saved.

Mimi nikapeleka maombi ya kuondoa Notice of Appeal iliyopo Court of Appeal kwa kutumia uamuzi wa msajili.

Baadae mdaiwa akaamua kulipa lakini alivyokuja kulipa akalipa akiwa amekata na makato ya NSSF japo kule NSSF hakupeleka, alivyoleta ule mkataba wa kuseto nilikataa kusaini kwa kuwa baadhi ya fedha hazijalipwa.

Na kweli malipo yote aliyolipa hakuna maandishi yoyote yanayoonyesha alilipa hizo fedha kwa madhumuni gani zaidi ya bank statement kama itahitajika.

Sasa wakili wake ananiambia niende mahakamani kudai hizo fedha alizokata na mimi nimemwambia siwezi kufungua kesi mpya wakati ile ya Corut of Appeal ipo na hakuna settlement agreement yoyote tulisaini mahakamani.

Swali je niendelee kukazia hiyo hukumu au nitaieleza Court of Appeal kuwa alilipa lakini hakupeleka baadi ya makato aliyokata kutoka kwenye hayo malipo? Maana zote hakupeleka NSSF zangu alizokata na za kwake alizotakiwa kuchangia.

Naomba msaada
 
Back
Top Bottom