Utekekezaji wa maagizo ya Bunge kuhusu ripoti ya CAG, PCCB nayo ikague mchakato wa kufanikisha mkataba wa DP World

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,214
3,587
Nyumba ya Mfalme/ Malkia inapaswa kuwa safi 100% pasina chembe ya shaka.

Huwezi kutibu Kisonono ukaacha Kaswende ukasema mgonjwa amepona aruhusiwe.

Wakfu wa uongozi mkuu unapaswa kutunzwa kwa 100%.

Vitani askari wakipoteza medani Kamanda ndiyo huadhibiwa. Kamanda anabeba wajibu wa makosa yake na makosa ya wapiganaji wake.

Kwenye soka timu ikipoteza mechi Kocha ndiyo anafungashiwa virago vyake.

Anapopanga timu analindwa na kinga ya kutoingiliwa na mtu awaye yote, timu ikipoteza mechi mkataba wake hautambui ile kinga.

Ndiyo maana wasiopenda matatizo naye huwa hawamuingilii anapopanga timu ila wanamsubiri kwenye matokeo.

Hapa ndipo Kocha anapogundua kwamba kumbe kinga yake iko kwenye kugawa namba tu (kupanga kikosi) ila anaowapanga wanaweza kumlipiza uwanjani (wanamvua kinga kwa kukosea uwanjani ili uongozi wa timu umuwajibishe kwenye mkataba).

Utekekezaji wa maagizo ya Bunge kuhusu ripoti ya CAG, napendekeza PCCB nayo iagizwe na Bunge kukagua mchakato wa kufanikisha mkataba wa DP World ili utekelezaji wa ripoti ya CAG uende sambamba na utekelezaji wa ripoti ya PCCB kuhusu DP World.

Palikuwa na tetesi za maafisa, wasanii na waheshimiwa Wabunge kupofushwa macho na akili ili mchakato wa DP World ufanikiwe.

Kusafisha nyumba ya Mfalme/ Malkia inabidi kona zote za nyumba zifagiliwe na watumishi wote wakaguliwe na wanaothibitika kukengeuka na kuupaka Ufalme matope wabatizwe upya kwa hatua za kinidhamu.
 
Hao bila maandamano mengine yote ni kelele za chura tu:

Kuwakamata Mwabukusi au Mdude hakutasimamisha maandamano 9/11
 
Back
Top Bottom