Utawezaje kumuamsha aliyelala ukiwa umelala?

Utawezaje kumuamsha aliyelala ukiwa umelala?

Franswar

Member
Joined
Feb 5, 2017
Posts
18
Reaction score
45
Utawezaje kumuamsha aliyelala ukiwa umelala? Kamwe huwezi kumuamsha aliyelala ukiwa umelala ni lazima kwanza uwamke ndo uweze kumuamsha aliyelala.

Hivyo hivyo kwenye biashara na ujasiriamali hii falsafa pia inatumika na kwa wale wanaotumia ndio pekee wanaofanikiwa katika malengo yao ya biashara na kwa wale wasio ifata wanabaki wakilalamika na kulaumu hawapati msaada kwa watu waliowategemea kuwapa misaada katika biashara zao au mawazo yao ya biashara.

Ukweli ni kwamba watu waliofanikiwa ktk biashara zao ni sawa sawa na mtu aliyepo usingizini kwani hakuna starehe kubwa kama usingizi na mtu akishakuwa usingizini haitaji usumbufu ndio maana mtu anayetaka kulala atahakikisha kwanza vile vyote vitakavyomsumbua wakati amelala havitamsumbua mfano atazima simu au kuweka silince, atazima radio, tv au kupunguza sauti.

Usingizi ni mzuri kwa tajiri ila kwa maskini ni mbaya. Ukisoma methali 24:33-34 Bado kulala kidogo,kusinzia kidogo,Bado kukunja mikono upate usingizi!Hivyo umaskini wako huja kama mnyang'anyi,Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha.

Kwa iyo tunaona kabisa hata Biblia inaonyesha kupenda usingizi ndio chanzo kikuu cha umaskini.Tajiri mpaka kawa tajiri aliacha kwanza kupenda usingizi.

Kuna utofauti kati ya kupenda usingizi na kupata usingizi, mara nyingi mtu anayependa usingizi mda wowote anapata usingizi haijarishi yupo mahali gani. Mtu asiyependa usingizi hupata usingizi akiwa amechoka kutokana na kazi au shughuli aliyofanya kwa mda mrefu hivyo humpelekea kupata usingizi na hatimaye kulala kwani kulala ni njia ya mapumziko kwa mtu aliyechoka

Kwa iyo ukipenda usingizi hata kama haujachoka utalala.Hapa ndipo umaskini wako utakuja kama mnyang'anyi na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha.

Tuludi kwenye swali letu utawezaje kumuamsha mtu aliyelala wakati wewe umelala? Kwa ufafanuzi niliyoutoa tunaona kwamba ukimuona tajiri kalala ujue kachoka kutokana na kazi alizofanya na anahitaji kupumzika na ukimuona maskini kalala ujue anapenda usingizi.

Sifa kuu ya usingizi haipendi kelele iweje upende usingizi wakati kichwani una kelele nyingi za ada ya watoto, kodi ya nyumba, chakula, bili ya maji n umeme na mengine kibao apa ndipo kwenye utofauti kati ya tajiri na maskini.

Maskini atasikia hizi kelele lakini ataziba masikio yake asisikie ili apate usingizi lakini tajiri atatega sikio azisikie vizuri hizi kelele ili ajue zinataka nini azipatie hapa tajiri ndipo anaposhindwa kupata usingizi na atapata usingizi endapo atazipa kinachotaka aya makelele yaweze kutulia kichwani mwake.

Na maskini siku akichoka kuziba masikio na mikono yake asisikie aya makelele ndipo anapojikuta bado makelele yanaendelea tena kwa sauti kubwa.

Yote kwa yote nilikuwa namaanisha kwamba tuache kulalamika hatuna mitaji ya kufanya biashara, ajira hazipatikani, serikali haitujali, mikopo siyo rafiki nk.

Tukiendelea kulalamika hivi ni sawa sawa na mtu aliyelala amuamshe mtu aliyelala = hakuna atakayeamka na pia ni sawasawa na kuziba masikio kwa mikono ili tusisikie makelele lakini mikono itakapochoka kuziba masikio utaendelea kusikia tu makelele tena kwa sauti kubwa HATUNA MITAJI YA BIASHARA, AJIRA HAZIPATIKANI, SERIKALI HAITUJALI, MIKOPO SIYO RAFIKI NK. Amka sasa upiganie ndoto zako zitakazomuamsha tajiri akusaidie.

Jua kwamba ata Mungu alivyokuwa anamuumba binadamu kwa kutumia udongo alichafuka mikono kwa kushika udongo sasa wewe umekuwa nani utaki kuchafuka mikono? Wakati aliyekuumba alichafuka mikono alivyokuwa anakuumba.

Kubali kuchafuka mikono acha kulalamika amka pigania ndoto zako. Mali hupatikana shambani udongo uliyokuumba ulipatkana shambani, nguo uliyoivaa (cotton) inapatikana shambani, madini yote yanapatikana shambani, kila kitu unachokiona kwenye macho yako kimetoka ardhini chuma, plastiki nk. Siri ya mafanikio ya kweli ipo shambani.

[HASHTAG]#Ontalio[/HASHTAG], mshana jr
 
Back
Top Bottom