Good Thinking Comrade.
Mada kama hii Jamii Forums, si mada pendwa. Tu wepesi mno wa kuchangia mada pendwa ambazo utamu wake huwa ni wa kitambo kidogo tu. Ngoja nidodose kidogo...
Today is your future. Maandalizi bora ya sasa ni mavuno bora ya uzeeni. Pia ya kusimulia uzeeni hupandwa leo. Iwe bora au duni, nzuri au mbaya.
Tuandae material things vya msingi, Asset za maana na kadhalika. Mjukuu akikuta viwanja, apartment za maana, maktaba iliyosheheni vitabu, ghala za kuhifadhia nafaka....itafana mno. Si akute Library za CD's za bongo movie, sub woofer za kila aina na orodha inaendelea..
Akute Autobiography yako, iso na ujanja ujanja ndani. Aisome na kuing'amua. Asikute vyeti feki. Akute tuzo mbalimbali za kijamii na kielimu na mengine mengi ya dizaini hii.
May almighty God strengthens all of us.
Asalaam.