Utata mtupu

yenyewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2014
Posts
621
Reaction score
94
John ni rafiki yangu sana, anaishi Dodoma wakati mi naishi Kahama. Huwa nampa story kuhusu mchumba wangu. Pia mchumba wangu nshawahi kumwambia nina rafiki anaitwa John lakin hawafahamiani.
Juzi John alikuja Kahama. Tulikutana tukapiga story kidogo.
Jana nkapokea simu kutoka kwa mchumba, anasema akiwa anazunguka mtaani kasikia mtu anamuita. Akajitambulisha kuwa ni John, anadai hakuamini ikabidi mchumba wangu ampe namba ya simu ili ahakikishe kuwa ni yeye.
Aliponipa hizi habari ikabidi nihoji kwanin anatoa namba haraka ivo.

YALIYONIFANYA NIONE UTATA
* mchumba wangu kutoa namba ya simu haraka, inawezekana ni mgawaji mzuri wa namba.
* leo nimekutana na John, tumeongea mengi lakini hajanambia lolote kuhusu kukutana na mchumba wangu na mimi sijamuuliza. Inawezekana kuna ajenda ya siri.

Mwenye lolote naomba anishauri kabla sijammwaga binti wa watu maana huwa sina moyo wa kuvumilia upuuzi.
 
Wabaki kugombea mpunga..........wenzio wala ndege alokula mpunga.........
 
Preta fafanua please
 
Last edited by a moderator:
Ukimwaga wenzio watamzoa
 
Kwani John anajua sura ya mpenzi wako? Au huyo mpenzi wako alitoaje number yake Kama pipi? Sikia kaa na Rafiki yako mweleweshe kabla haijafikaa mahali mkakosana bint asiwachanganye akili zenu...
 
Kwani John anajua sura ya mpenzi wako? Au huyo mpenzi wako alitoaje number yake Kama pipi? Sikia kaa na Rafiki yako mweleweshe kabla haijafikaa mahali mkakosana bint asiwachanganye akili zenu...

Alikuwa ata hajawahi kumuona. Nahisi kuna mtu kati ya aliokuwa nao alimwambia.
Mimi naona bora niachane na huyu binti ili asiharibu urafiki wetu na huyu jamaa maana tumetoka mbali sana. Kutoa namba kirahisi ivo inaonesha huwa anawapa wengi.
 
Shida nyinyi wanaume mnapendaga kutambiana sana oooh demu yuko hivi, mala demu yuko vile namt..ba hivi au vile! hapo naona ipo kitu umemfanya huyo John kufanya kila njia na kumsaka huyo demu wako. Jipange upya yenyewe na domo lako ulicontrol, maisha ya sasa NO and i repeat NO BODY TO TRUS, TRUS YOURSELF.
 
hivi simu ina nini mpaka iwazidi watu akili ??
 
hawafahamiani, wamekutana mtaani dem akaitwa jina(HOW) na akatoa namba(WHY)
shemeji unachezewa kekundu na hao mafalah rafiki ako na huyo dem wako
 
Nimekuelewa sana
 
Kwani huyu John ni yule john mtembezi au john kisomo?
 
hivi simu ina nini mpaka iwazidi watu akili ??

Kwi kwi kwii.. hizi nyuzi za simu zishakua nyingi hapa.. Nadhani jamaa anataka kwenye simu ya demu wake kuwe na namba yake tuu demu akitoa namba kwa mwingine inakua kesi..
 
johny wa aladee kawagonganisha mambo kataka kuonja asali ya shem.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…