Utaratibu wa kulindwa na polisi nyumbani

Kibundi wa getto

JF-Expert Member
Sep 28, 2013
455
877
Wakuu
Mimi nauliza utaratibu ukoje Kwa mtu binafsi akitaka kulindwa na polisi nyumbani kwake.

Je kuna gharama zozote ambazo itanibidi nilipie?

Au ni nani mwenye mamlaka ya kunipa huo ulinzi wa polisi nyumbani?

Na katiba inasemaje kuhusu ulinzi wa polisi Kwa Watu binafsi?
 
Muulize Babu tale na Diamond wakueleze wale FFU pale madale Wametoa wapi
 
Hata unaowaona wanalinda kwenye Mabenki, zile bank zinalipa.
Nakushauri uende kwa OCD wa sehemu ulipo akupe maelezo ya kushibisha
 
Kwa swala la kutekwa ikibidi kufanyinka hao hao utakaokuwa unawalipa watapewa maelekezo toka juu wakuteke. Ni sawa na kukaa na simba nyumbani kwako ukitegemea asikule nyama.
Hahaha hahaha kama kuna ukweli hivi. Ila watekaji wako wa aina nyingi bhana
 
Tunaona mabenki yanalindwa na FFU kama CRDB na NBC....lakini pia watu au makampuni yanapewa escort na jeshi la polisi ili kubeba pesa zao...kwa malipo maalum...ila sijawahi kusikia kama inawezekana kulindwa nyumbani kwa mtu binafsi....hebu kamuulize yule kibibi gagula wetu ..atakua anajua tu
 
Back
Top Bottom