daniel merengo
JF-Expert Member
- Aug 19, 2011
- 277
- 98
Kwa ufupi
Alisema baada ya kupata taarifa hiyo, alikwenda karibu na hoteli hiyo kuchunguza ukweli wa jambo hilo na kabla ya kuingia ndani alimwona mtuhumiwa akiwa na mtu mwingine ambaye hakumtambua akishuka kutoka kwenye gari.
Dodoma
Mkutano wa maridhiano uliokuwa umepagwa kufanyika jana mjini hapa kati ya CCM na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) umeshindikana huku mwandaaji akitapeliwa Sh400,000.
Mkutano huo ulipangwa kuwashirikisha viongozi wastaafu wa ngazi za urais na waziri mkuu na ulikuwa ukiratibiwa na Kituo cha Kulea Watoto Yatima cha New Hope Family cha mjini hapa.
Mmoja wa waratibu wa mkutano huo, Omary Kombe alisema kusitishwa kwa mkutano huo kulitokana na taarifa walizopewa kwamba viongozi hao wasingeweza kupatikana kutokana na kupewa taarifa ya muda mfupi.
Kombe alisema tayari wahusika wote walikuwa wamearifiwa na baadhi ya mahitaji yalikuwa yamelipiwa zikiwamo Sh400,000 zilizotolewa kushika ukumbi katika Hoteli ya Dodoma, ambazo baadaye zilikuja kutapeliwa.
Fedha hizo zilizua mtafaruku jana baada ya mmoja wa washirika katika maandalizi ya mkutano huo kuzichukua kinyemela kutoka uongozi wa Hoteli ya Dodoma bila wenzake kufahamu.
Kombe alisema jana asubuhi alipigiwa simu na mtuhumiwa huyo akimwambia kuwa asifike katika Hoteli ya Dodoma, kwamba angekamatwa kwa kuwa kulikuwa na askari wengi hotelini hapo.
Alisema baada ya kupata taarifa hiyo, alikwenda karibu na hoteli hiyo kuchunguza ukweli wa jambo hilo na kabla ya kuingia ndani alimwona mtuhumiwa akiwa na mtu mwingine ambaye hakumtambua akishuka kutoka kwenye gari.
Alisema aliamua kwenda polisi kutoa taarifa na alipofika alimkuta mtuhumiwa kituoni hapo akikabiliwa na tuhuma nyingine za utapeli wa kutolipa fedha za malazi kwenye nyumba ya wageni. Mtuhumiwa huyo alipohojiwa na polisi, alisema yeye ni mjumbe wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa Dar es Salaam. Hata hivyo, Katibu wa UVCCM mkoa huo, Kisamba Kidando alisema hamfahamu na hayumo katika orodha.
Kamanda wa Polisi Dodoma, David Misime alisema wanamshikilia mtuhumiwa kwa utapeli.
CHANZO: Mwananchi