Utapeli huu unaendelea

ngoshwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2009
Posts
4,141
Reaction score
951
Ule utapeli unaohusisha vijana wa kitanzania mwingine ana rafudhi ya kihaya anajiita Josepph Martin na Mwingine mbantu anaejifanya Mzungu (Mjerumani) unaendelea kwa staili ile ile ya kukupigia simu, wanajitambulisha kuwa wanakufahamu, wanakufahamu kwa kukutajia hata rafiki zako wa karibu au wenzio wa ofisini. Walianza kwa kutapeli kuhusu biashara ya Madawa ya Mifugo na wanyamapori..

Episode 2: sasa wanakuadaa kukupa kazi kwenye Kampuni yao inayojishughulisha na Ujenzi wa vituo vya watoto yatima (orphanage Centers), rafiki yangu amenisimulia wamemkosakosa muda mfupi uliopita kilichomsaidia ni kuzitambua namba zao za simu kupitia mfumo wa kujaribu kutuma pesa na akagundua huyo Joseph Martin jina lake ni Josephat Haule na huyo anaejifanya mjerumani ni Revocatus Mbande. Inashangaza sana kuona hakuna hatua za makusudi zinafanyika kupambana na utapeli huu unaoonekana kushamili nchi! Vyombo vya dola kimya, makampuni ya simu kimya na Tume ya mawasiliano kimya kabisa!.
 
..., wewe uwe wakwanza kuchukua hatua, ukimshirikisha huyo rafiki yako. Nenda ukatoe taarifa kwenye ofisi za mtandao wanaotumia, watasaidia kuwapata hao matapeli.
 
..., wewe uwe wakwanza kuchukua hatua, ukimshirikisha huyo rafiki yako. Nenda ukatoe taarifa kwenye ofisi za mtandao wanaotumia, watasaidia kuwapata hao matapeli.

kuna tapeli mmoja tayari ametiwa mikononi mwa Dola na ameshashughulikiwa kinoma jana jioni.
 
Jamaa yangu Arusha walimtoka 5M last year... hawa jamaa basi tu!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…