Utamu wa Vumbi la Coco.....

Kasie

Platinum Member
Joined
Dec 29, 2013
Posts
22,805
Reaction score
43,230
Habari ya siku mbili tatu waungwana....
Poleni na maombolezo ya msiba wa kivuko cha MV NYERERE.

Basi tuendelee na Mahaba ya Kasie.

Wiki mbili zilizopita nilikuwa bongo daslama na hapo ndo nikajua kumbe vumbi lina utamu wake eeeh hehehehee.

Kwa kinywa chake kanitamkia hivi, wee mla vumbi kumbe mtamu hivii basi nikabaki natabasamu na kurembua macho huku nikiuma uma midomo.

Kati ya wiki mbili hizo zilizopita tarehe moja wapo ilikuwa ni kumbukumbu yangu ya siku yangu ya kuzaliwa. Huyu bana anajua siku yangu ya kuzaliwa kumbe yeye alipanga aje anifanyie suprise birthday ila sio party yaani tutoke mie na yeye tuu kama Sea wa Mivalo na mpenzi wake.

Basi nikamwambia tarehe flani nakuwa Dar, na yeye akatoka alikotoka akaja Dar tukakutana. Mie sina hili wala lile kuhusu birthday maana nlishaacha kusherehekea siku ya kuzaliwa, ikitokea nikikumbukaga basi huwa naenda kutoa sadaka inapit, nikisahau maisha yanaendelea.

Sasa ilivofika siku ya tukio huyo jamaa wangu wangu hadi kiwanja kimoja hivii kimetuliaa tukapata kuanzia breakfast buffet, mlooking wa mchana na jioni tulikula bites, nyama choma na hard liquor. Usiku mnene tukaenda kuukemea uzee hukoo club moja ya malegendary hadi usiku mnene.

Tukapata hewaa / break siku kadhaa baada ya kunutoa out, akaniambia anataka arudi kwao nikamwambia kabla hujaondoka naomba nikutoe out bill on me.

Basi nikampitia alipofikia huyoo tukaelekea coco beach. Beach kongwe tangu miaka hiyoooo tuko chuo. Kufika eneo la tukio magabacholi wako kibao na familia zao wanakula upepo wa bahari. Mbio vijana kadhaa wakatukimbilia wakitukaribisha bidhaa za pale kila mtu tununulie kwake. Basi mmoja wapo akafanikiwa kutushawishi akatupangia viti na meza, daah kwa macho meza hazivutii kuweka chakula hapo ila ndo mazingira hayo. Jamaa akataka tuondoke kwani akasema hatoweza kula hapo, nikamwambia tafadhali naomba uniruhusu mie nile halafu tutaondoka nikupeleke ukale kuku wa kuchoma uhindini.

Nikaagiza mhogo mmoja na mishkaki portion moja. Ukaja muhogo wa motoo na kachumbari na chachandu kwa juu asaalaaleeh. Muhogo lainii unanyambuka kama chapati za bi Fatuma heheheh na mshkaki ikaja na sosi tamu hilooo duuh acha tuu. Kipindupindu weka pembeni chakula cha vumbi kitamu bwana.

Nikanawa halafu nikaanza kula, nikamwambia naomba nikulishe kidogo ukiona taste mbaya temaa maana chini ni mchanga. Kishingo upande akakubali, nikamlisha kipande cha mhogo nilichochovya chachandu kachumbari na mshkaki. Hahahahaha ukiwa na misimamo yako usijaribu kushawishika kuonja, huachii. Ndo kilichotokea jamaa.

Nikamuangalia nione atatema au atameza, weeh vikateremka hadi tumboni aahahahahaa si mchuziii huooo.

Nikamuagizia mhogo wake na portion yake ya mshkaki ikaja akanawa akaanza kula. Aliongeza na kuongeza na kuongeza kama round 4 hivi. Nikamuagizia na juice ya miwa ya moto na yenyewe alitilia mashaka ila baada ya kuonja akaongeza glass nyingine 3.




Meza ya vumbi ikachafuka kwa msosi wa wala vumbi. Ila utamu wa hivi vyakula vya anina hii havifikii utamu wa vyakula vya subway wala Pizza Hut huko maana vyote nshakula.


Tulijikuta tumekaa hapo hadi kagiza kakaingia mie nikaanza kusikia baridi nikamwambia twende bana mie nasikia baridi..... Kifuatacho ITV.....


Jamaa akanogewa na kuchukua take away.......


Asubuhi ananiambia kumbe wala vumbi ni watamu hivyo eeeh...... Na vyakula vyenu ndo kabisaa.

Basi mie natabasamu tuu na macho kumchuzi.
Usishangae mtu na usafi wake anafata wanawake wala vumbi, vumbi lina utamu wake. ....ile chumvichumvi ile....

Ila ..........kuna tofauti ya vumbi na uchafu..... usichanganye tafadhali.

Kasie Mahaba Matata.
 
[emoji23][emoji23][emoji23]mi nikawaza vumbi la congo tu.

Kimoyo moyo nikasema kumbe Coco nako kuna vumbi lake..

Mmh haya
 
[emoji23][emoji23][emoji23]mi nikawaza vumbi la congo tu.

Kimoyo moyo nikasema kumbe Coco nako kuna vumbi lake..

Mmh haya

Hahahahahahaaa nilijua tuu watu watawaza mavumbi mengine, hili ni vumbi vumbi la mjini daslama aka Coco Beach.

Ile mihogo ni mtamu asikwambie mtu.
 
Aaagh mm nilijua kasongo bhana kumbe dah.
Anyway hongereni kwa goodtime.
 
nikitaka kusema sasa casie matata vumbi la congo yeye kapaka sehemu gani πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

kumbe coco nako kuna vumbi
 
speaking of wala vumbi miaka kadhaa nyuma nikiwa 21-23 yrs UNI/COLLEGE days

katika harakati za ujana nilibahatika kuibukia club moja ipo temeke Girafe club/Royal club

bwana wee nilijikuta kila weekend nipo pale siyo kwa sababu ya mziki mzuri ila ni wale wasichana wa temeke

naungana na mdau wa casie matata wala vumbi ni watamu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Sasa mbona umeacha interesting part.

Ila kweli tuendako ni pabaya, zaman mtoto wa kiume ndo anahadithiaga alivogegeda. Now mtoto wa kike pia anahadithia alivopewa mautami
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…