Utamkaji wa neno Tanzania

Mwanitu

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2010
Posts
1,035
Reaction score
597
Nimekuwa nikisafiri na ATCL mara kwa mara. Nimekuwa nakerwa na watangazaji wao wa flights wanavyo litamka jina la Taifa letu.

Wengine Air Tanzenia,
Wengine mkazo sivyo.Wageni wanashangaa nchi inatakwa tofauti tofauti.

Hebu tujitahidi kutamka lilivyo sahihi.Sijawahi kusikia nchi nyingine ikiwa inamatamshi mengi kwa nchi moja.Inachanganya wageni
Hata wasijui tamshi lililo sahihi.
 
Wanaiga wazungu sio? Tanzenia ni nini? Hatujitambui, badala tuwarekebishe, na sisi tunawaunga mkono katika kulitohoa jina letu, kisa ni weupe, kila walifanyalo ni sahihi!
 
Kwani sisi huwa tunatamka vizuri majina ya nchi nyingine? kama vile sisi tulivyoamua kuiita Moçambique 'Msumbiji' basi tusilielie wengine wakituita Tansaniee
 
Kwani sisi huwa tunatamka vizuri majina ya nchi nyingine? kama vile sisi tulivyoamua kuiita Moçambique 'Msumbiji' basi tusilielie wengine wakituita Tansaniee
Wahudumu wa atcl wanatoka nchi gani? Nisishangae na kuuliza, pengine ni wa Rwanda, si ndio waliotupa hata wazo la kununua ndege?
 
Wahudumu wa atcl wanatoka nchi gani? Nisishangae na kuuliza, pengine ni wa Rwanda, si ndio waliotupa hata wazo la kununua ndege?
inawezekana wahudumu wakawa wazawa lakini pilot in command na cockpit crew yake inaweza kuwa na wageni wakutosha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…