joshydama
JF-Expert Member
- May 10, 2016
- 4,623
- 5,039
Nawasalimu wote familia ya MMU,
Wanawake/wasichana ni nani aliyewaambia kuwa kila mahusiano mnayoyaanzisha lazima mwisho wa siku yazae ndoa?
Kwani hamuwezi kuanzisha uhusiano kwa ajili ya kupeana raha au kampani tu? Ni lazima uliyenaye katika uhusiano wa kimapenzi akuoe?
Baadhi ya wasichana/wanawake wamekuwa wakiingia katika uhusiano wakiwa na malengo makubwa ya kuolewa. Hivyo basi inapelekea muda wote kuuliza hili swali mara kwa mara.
Ni lini utanioa au unampango gani na mimi? Kiukweli huwa mnakosea sana kuuliza hayo maswali kwa sababu ishu ya ndoa siyo ya kuulizauliza bali mhusika mwenyewe ndiyo inabidi yani mwanaume atangaze ndoa.
Hayo maswali yenu huwa mnategemea mhusika atakwambia sitokuoa au sina mpango wowote akukose. Siku zote utapigwa saundi kubwa ili ukae laini akufaidiwe ipasavyo na akiona umechoka anakupiga chini anachukua kifaa kingine kipya. Unabakia kuwachukia wanaume na kuwaona watu wa ajabu wakati hatuko hivyo.
Na wengine huwa wanaenda mbali zaidi mpaka kutegesha apewe mimba ili iwe ndiyo tiketi ya ndoa. Poleni sana.
Siyo wewe mwanamke au msichana muda wote kulazimisha kuolewa. Kiukweli siyo fresh sana kulazimisha ndoa. Nawaomba mbadilike na muache hiyo tabia.
Siyo lazima unayekwichikwichi naye mwisho wa siku akuoe wengine huwa wanahitaji tu kufurahisha miili yao na kupata faraja.
Au ndoa ndiyo mnaona ni dili sana katika maisha yenu? Kuna mambo mengine makubwa tena hata zaidi ya maisha ya ndoa ingawa siyo kwamba nawashauri muache kuolewa bali msipende kulazimisha kuolewa.
Mkipunguza suala la kulazimisha ndoa hakika nawaambieni single mother watapungua mtaani.Naomba mtambue kuwa Wengi wetu sisi wanaume huwa hatupendi kulazimishwa katika suala la ndoa.
Kwanini mnapenda kulazimisha kuolewa?
Je ndoa ndiyo kitu pekee ambacho mnakiona cha muhimu na maana kuliko vitu vyote hapa duniani?
Karibuni kwa maoni yenu!