Utalii wa Tanzania

mtafiti muelewa

Senior Member
Oct 16, 2013
186
98
Kumekuwa na wimbi la jirani zetu (WAKENYA) kujimilikisha kwa maneno vivutio vyetu vya utalii. Si sahihi na si haki kwa wao kufanya hivyo. Lakini kuna kitu huwa najiuliza. Je ni jitihada gani zinachukuliwa na mamlaka husika juu ya hili? Au wameridhika kwa kuwa Tanzania inachukuliwa kama shamba la bibi?
Kwanini hatusikii wizara husika ikitoa matamko?
Serengeti yao, Kilimajaro wao, Olduvai Gorge iko kwao pia. Sitoshangaa siku wakisema hata Zanzibar iko kwao.

Mimi nadhani vitu viwili vifanyike.

Mosi: Serikali itoe tamko juu ya hawa jirani kuwa waacha kuudanganya ulimwengu. Waseme walivyonavyo na vyetu watuachie.

Pili: Mamlaka husika lazima ijue kuwa biashara haiishii kwenye bidhaa bora tu. Inakwenda zaidi ya hapo. Ile dhana ya kizuri cha jiuza imeshakufa. Lazima wavitangaze vivutio hivi kitaifa pia kimataifa. Si hata chembe ya shaka 90% ya watanzania hawajui hatá gharama za kupanda mlima Kilimanjaro, hawajui kiingilio Ngorongoro ni bei gani.
Hili ni tatizo.
Tusipo tatua tutaendelea kuwa SHAMBA LA BIBI DAIMA.
 
Wakenya hawajui serikali isiyojali ya mjomba JK ilishamaliza muda wake?
 
Majarida ya kimataifa yapo,tv za kimataifa zipo,tutangaze vivutio vyetu huko.
 
Majarida ya kimataifa yapo,tv za kimataifa zipo,tutangaze vivutio vyetu huko.
Kweli mkuu. Sasa sisi tumekaa kaa tu tunasubiri. Wenzetu wanatumia hadi udanganyifu kupiga bao. Sisi wenye navyo kweli tuna toa toa macho tu.
 
Back
Top Bottom