Kwanza kabisa usafir ni wa boti ama ndege..kama utatumia boti nauli ni 25,000 economy seat 35,000 ni business class na 70,000 ni VIP nauli ya ndege cjui kwan inabadilika badilika. Ukifika Zanzibar unatakiwa kujua kua utakua mjini au shamba, na shamba ndio kumetulia na wagen wengi wanakwenda huko. Shamba zilizochangamka ni Nungwi, Paje, kiwengwa, michamvi, na kizimkazi..suala la kuona dolphin ni kizimkazi kwan kuna dolphin wengi huko pia kama unapenda snorkeling nenda Nungwi kuna kisiwa kinaitwa Mnemba watu wengi hasa wagen kutokea mataifa mbali mbali huwa wanakwenda Mnemba kwa ajil ya Snorkeling.Pia kuna spice tour hii ni kwa ajil ya kutaste Zanzibar spices (viungo vya Zanzibar hasa karafuu) pia kuna mambo ya kihistoria mengi kama Ngome za waarabu na majumba ya kale huko utaona Beit al ajaib ipo stone town pia kuna Ngome kongwe ambapo kunafanyikaga sauti na busara festival na shughuli nyingine hasa Zanzibar music. Kuhusu maakul jion usikose kuhudhuria forodhani na kama wewe ni mtu wa muzik nakushauri usikose kuenda Nungwi maeneo ya kendwa for full Moon part pia Nungwi kuna night club nyingi Sana maaruf ni cocobello ikifatiwa na cholo bila kusahau jtano usiku wa reggae party hakika utainjoy na kama hauna company ni pm hahaa.Karibu Zanzibar hakuna matata