Utakuwa umemsaidia mtoto wako sana akijua Kichina kuliko lugha yako ya asili

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,577
15,338
English na Kichina (Mandarin) utake usitake ndizo lugha ambazo zinatawala na muda sio mrefu Kichina itakuwa lugha ya dunia sawa na Kiingereza.

Ukizunguka jijini ni mambo machache tu ambayo hayana mkono wa Mchina.

Acha kumkomalia mtoto wako ajue Visukuma, Vihaya, Viarabu na Vindengereko. Hivyo mpeleke kwa bibi yake huko atajua automatically ila mpeleke akajifunze Kichina ili awe raia wa dunia ijayo asiyepwaya.

Sisisitizi Kiingereza kwa sababu najua hata masikini aliye kijijini anatamani akijue.

Mtu anayejua lugha za kidunia anafaida ya ziada kwa anayejua lugha za kienyeji na Kiswahili tu.

Nimemaliza, kama inaleta maana ifanyie kazi mkuu. Tatizo la wazazi wengi hatupendi kuona watoto wanatuzidi.
 
Kuna airport fulani huko mkoani nilisikia matangazo yanatangazwa kwa lugha 3....kiswahili,kingereza halafu wanamalizia na kiChina

Kimsingi kujifunza lugha za mataifa mengine ni jambo la muhimu kwasababu huwezi kujua utaitumia katika mazingira gani....nikipata chance nitajifunza zaidi
 
Back
Top Bottom