Utajiri wa kichawi

D Metakelfin

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2017
Posts
3,728
Reaction score
4,181
Wakuu
HABARI zenu na imani wengi mu wazma wa afya na mnaendelea vyema na majukumu ya kimaendeleo na kwa wale ambao sio wazma poleni sana nawaombea mpone na muendelee na shughuli zenu

Takribani miezi sita iliyopita rafiki yangu mpendwa ambae sitamtaja jina alipatwa na msiba wa kuondokewa na mdogo wake wa kiume ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa kidato cha nne akiwa amebakiwa na mda mchache afanye mtihani wake wa mwisho.
Kwa kweli mimi nilikuwa mmoja ya watu tulioumizwa sana na kifo hicho ukizingatia siku moja kabla ya kifo hicho kutokea nilimuona marehemu akiwa mzma wa afya.
Siku ya msiba wazazi wa marehemu walilia sana ikafikia hatua mpaka mama wa marehemu kupelekwa hospitali kwani alikuwa akipoteza fahamu mara kwa mara baba wa marehemu nae alilia mpaka macho yakamvimba.
Lakini wakuu kitu kinachonishangaza na kunipa maswali ni utajiri wa ghafla ulioanza kuchipua mara baada ya kifo cha mtoto huyo.Walikua wakiishi katika nyumba ya kawaida tena ya hali ya chini lakini sasa wamezungushia uzio pia wameweka umeme na maji na hivi karibuni wamenunua hiace na gari ndogo(forester used).
Najua wengi mnaweza kudhani labda ni jitihada zao binafsi lakini nadhani mapato yao ni tofauti na mali walizoanza kuzimiliki baada ya kifo cha mtoto huyo.
Baba ni dereva hiace na mama anauza mgahawa huko uswahilini.
Wakuu sidhani kama kweli kwa akili mlzonazo ma-greater thinkers mnaona mali hzo znaendana na kazi hizo.
Zaidi namsikitikia mtoto huyo kwani nadhani ndiye mzalishaji wa mali hizo huko katika ulimwengu wa giza.
wale msioamini uchawi mpo?
Wanaoelewa zaidi kuhusu mambo ya giza nadhani mtatuongezea elimu zaidi
Sipendi povu
 
Wewe K NI K Kwanini Umewaza moja kwa Moja katika nguvu za giza hujawaza Labda kuna jambo jingine limewapa neema? Kwani forester used ni bei gani?

Halafu unajua kuna Madereva daladala wanalala na faida mpaka laki moja kwa siku? fanya tafiti ndugu.

Siamini kama kun kupata hela kwa njia za giza. kwa usawa huu wa awamu ya tano tungepanga foleni kwa hao waganga kama ilivyokua kwa babu wa loliondio
 
Binadamu bhanah!.

Inakubidi kama ndugu yako akifariki, kama una mipango uliyopanga kutekeleza siku za Karibuni inakubidi usikitishe kwanza kwa sababu ukitekeleza tu wanajua umemuondoa wewe.

Hiyo ni mipango ya mufa mrefu tu ambayo huenda walipenda kuyatekeleza sasa. Bahati mbaya sana mtoto wao alifariki kipindi kifupi kilichopita, binadamu huanza chokochoko.
 
Mkuu biashara ya daladala ni ngumu sana na sidhani kama ni rahisi kununua hiace yako mwenyewe gari ya kutembelea,kujenga tena ni kwanini iwe baada ya kifo
 
Inawezekana kabisa mtu akapata utajiri wa haraka kabisa kwa kutumia njia za giza kwa kumtoa kafara mwanadamu mwenzio (hasa mtu wa karibu wa ukoo). Hata kwenye Biblia ipo mistari (wala sio mmoja) inayoonyesha kwamba kweli mtu anaweza kupata mali na vyeo kutoka kwa shetani.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…