Utajiri Wa Kenya Unatokana na Uzembe Wa WaTz

sonaderm

JF-Expert Member
Nov 9, 2015
618
1,816
Hivi juzi nimeona mijadala mingi kwenye mitandao kuhusu mmoja wa wakilishi wa kenya kusema olduvai gorge ipo kenya na alidai mwalimu wake ndio kamfundisha hivyo..Hili sio jambo geni ukizingatia ni mambo mengi siku za nyuma wakenya wame claim baadhi ya vitu kuwa vipo kenya!Kifupi ni jamaa kwa miaka kadhaa wanatembelea nyota na kupiga hatua sana kimaendeleo..Bila shaka hata la juzi kuna watz walikuwa hata hawajui kama kuna kitu kinaitwa olduvai gorge na historia yake..walimu mpo?

Nikirudi kwenye mantiki ya post yangu..Tatizo naliona sio kenya bali ni sisi watz ndio tuna matatizo hasa serikali yetu na idara zake kutofanya jitihada za kutosha kwenye kusimamia mambo na kuona opportunities..kwa mfano:

1. Kenya imepata mapato sana kwenye sekta ya bandari ya mombasa na hili ni kutokana na uozo uliokuwepo bandari ya dsm..hakuna ubunifu na miundombinu haijitoshelezi na ujanja ujanja uliokithiri..Juzi bandari ya mombasa imepanuliwa na infact ni kuendeleza ushindani na sisi!They are serious with the business (in jerry muro voice)

2. Madini ya Tanzanite imeonekana yanatoka kenya na yameifaidisha sana kenya..Serikali yetu imelala na hapa tutawalaumu wakenya?wacha kenya itambe!madini yanapita kwenye mipaka na hakuna kodi zozote zinazotozwa..hayo hayo madini yanayotoka tanzania ndio yamejenga flyovers kwao.

3. Lugha ya kiswahili..wakati watz wakijigamba kiswahili kimeanzia kwao wakenya wameongoza kwa kutoa walimu wengi wa kiswahili na kufundisha nje,wameandika vitabu na kukitangaza kiswahili kuliko watz..Tumebaki na sifa za kijinga tu kuwa tunawazidi wakenya kuongea kiswahili-so waht?.Idara zinazohusika zipo na hakuna la maana wanalolifanya zaidi ya kuongea propaganda za kisiasa!Infact tumelala na huwa tunastuka kwa muda na kurudi kulala tena..

4. Utalii ni sehemu ambayo hawa jamaa ndio wametembelea nyota miaka yote-Lakini bado mamlaka zetu zipo zipo tu!Tunalalamika na baada ya mida shughuli huendelea kama kawaida!lazima kuwe na mikakati endelevu juu ya kutangaza maeneo yote ya historia na vivutio..si ajabu pia watz wenyewe hatuna utamaduni wa kuyatembelea haya maeneo,je mgeni akija kukutembelea utaweza kumuelezea kuhusu hayo maeneo?ifike mahali kila mtz awe ni sehemu ya kutangaza ila lazima kwanza mamlaka husika zionyeshe seriousness ya kazi iliyopewa..Kuna jamaa mmoja alienda nje kwenye warsha kikazi na wakati wa kujitambulisha wakawa wanaulizwa wanatokea nchi gani na waelezee kuhusu nchi yao,jamaa akajitambulisha anatoka Tz na akaishia kutaja mlima kilimanjaro pekee wakati kuna vitu zaidi ya mia!

Kwa kifupi naona wakenya kama nchi inayotafuta fursa kwa maendeleo ya nchi yao ni sawa kabisa kuvuta upande wake maana sisi tumelala hasa serikali yetu na mamlaka zake..Na waendelee hivyo hivyo mpaka siku tustuke usingizini kiukweli kweli!
 
Pamoja na hayo jamaa wako vizuri na wala tusilalamike, wanatuzidi kila Idara, Shirika lao la Ndege ni kubwa sana na utalii wao kwa kiwango kikubwa unachangiwa pia na shirika lao la ndege. KQ.

Kenya kwenye nchi za subsahara ndo inaongoza kwa kuzalisha maziwa, sisi tuna maeneo makubwa ila tumabakia majungu tupu.

Kenya ndo nchi ya pili kwa kuwekeza Tanzania kwa kifupi jamaa wana investment nyingi sana tanzania kuanzia Mabenki, Mahoteli, viwanda, Mashule na kazalika sasa sisi tujilulze tuna vitega uchumi vingapi kenya?

Hahaaa tunedlee kulalamika jamaa wana paa, huumu da wa kulalamika ni bora watu tupige kazi maendelo hayaji kwa kulalamika bali kufanya kazi kwa bidii
 
Naona umesema bandari ya NAIROBI. Sina uhakika kama wamefanya upanuzi wa bandari kutoka Kenya kwenda Nairobi.
 
Bandari ya Nairobi basi hawa jamaa wapo vizuri, Kam Wana pesa ya kuongeza bandari toka Mombasa mpaka Nairobi. Kiukweli Kenya bandari yao kubwa ipo Coastal region Mombasa.. Nairobi hakuna port
 
Watakuja siku kusema Dar es salaam ni mji uliopo kenya tusipoangalia....aisee kiukweli tumelala sanaaa

mi nimeamua kuwalia denge.. hawatothubutu kisema tena eti hiki ni chao... kamwe..

ungana nami kwa ajili ya Tanzania yetu
 

Attachments

  • 1456830847103.jpg
    1456830847103.jpg
    42.5 KB · Views: 35
Uzi mwingine wa malalamiko kuhusu Kenya, iangalieni Kenya kwa jicho chanya kama mnataka maendeleo ya kweli
 
MAGUFULI:,my president;would you please mind concentrating on this for just a week and leave behind some other issues?.najua nguvu yako italeta tija hapa kwenye utalii na maliasili.
Hapa kwenye utalii nasikia ndiyo penye mzigo mkubwa kwenye uchangiaji wa pato la Tanzania,na ni hapa hapa ndipo panapofanya watoto wa kenya kuvimba masaburi hadi kusema waziwazi kuwa mali zetu ni zao,
Simama hapa kwa siku saba tu,fumua wizara/idara na kila kidudu mtu kilichopo hapa kwa miaka miwili kurudi nyuma wakapumzike kabisa.
wametupotezea mapato sana,wametuaibisha sana,wametudhalilisha sana,wameiba na kuuza mali
zetu sana,wamepokea asilimia kumi kutoka kwa jirani ili wawe mabubu sana,Ooooh sana imetosha sana!.Maana sasa hadi wewe watasema mkenya.
MALIASILI/UTALII kumeoza sana.
 
Back
Top Bottom