Utafiti wa wazi mitaani na kwenye mitandao ya jamii

mtunzasiri

JF-Expert Member
Dec 24, 2012
1,446
988
Je ni kweli chama cha mapinduzi kinajali raia wake zaidi kuliko ukilinganisha na vyama vya upinzani?

Je ni kweli dhamira na malengo yake ni kwa ajili ya nchi tuu na sio vyeo na madaraka binafsi zaidi, ukilinganisha na vyama vya upinzani?

Tafadhari unapojibu maswali haya toa na sababu zake karibuni.
 
Hakuna chama kinachojali wananchi. Siku zote vyama vinaangalia maslahi binafsi zaidi. Ndo maana chama kischo dola hupinga hata mazuri kwa sababu ya neno "upinzani".

Vyeo ndo kila kitu. Tumeona sana katika siasa za Tz. ZZK amekuwa mfano wa wale wanaonyamazishwa kwa shekeli.
 
chama cha kujali wananchi kwa 100% bado hata mimba yake haijatungwa achilia mbali kuzaliwa...
 
Umasikini na ubinafsi ndio chanzo cha mambo mengi hata kama chama kina sera nzuri lazima watatoka nje ya mstari.

Pia mfano kwa hapa bongo mfumo wa chama kimoja imekuwa ni Tatizo hivyo tumejikuta uvumilivu umetutoka kwa kusubiri ahadi zisizo tekelezeka zaidi ya miaka 50.
Kwa hiyo kila mtu akaanza kuchukua time zake kujiangalia yeye na familia yake.
Familia ya mwingine utakufa na njaa zako.
Akili za kupiga dili zikatawala na uzalendo kutoweka kabisa.
 
Hakuna chama kinachojali wananchi. Siku zote vyama vinaangalia maslahi binafsi zaidi. Ndo maana chama kischo dola hupinga hata mazuri kwa sababu ya neno "upinzani".

Vyeo ndo kila kitu. Tumeona sana katika siasa za Tz. ZZK amekuwa mfano wa wale wanaonyamazishwa kwa shekeli.
Kamfano ka jambo zuri linalopingwa na upinzani pliiiiiz!
 
Back
Top Bottom