Salahan
JF-Expert Member
- Sep 10, 2014
- 2,963
- 3,675
Facebook au Instagram inaweza kutufanya tuwe wapweke au wenye hasira kwasababu hujikuta tukijifananisha na watu wengine wanaonekana kuwa na maisha bora, utafiti mpya umebaini.
Mitandao hiyo inadaiwa kuwapa watumiaji mtazamo usio sahihi kuwa watu wengine wana furaha zaidi kuliko wao, watafiti wamesema.
Utafiti huo ulifanywa na taasisi ya utafiti wa furaha ya Denmark na kuhusisha watu 1,095. Walifanya utafiti huo kwa kuwaambia nusu yao kutotumia Facebook kwa wiki na nusu nyingine kuendelea kama kawaida.
Baada ya siku saba, wale waliojiondoa Facebook walikuwa na kiwango kikubwa zaidi cha furaha kuliko wale walioendelea. Wale waliojinyima na Facebook walidai pia kujihusisha na mambo ya ulimwengu wa kawaida na hawakuwa na hasira au kuwa wapweke kulinganisha na watumiaji wa Facebook.
Walibaini kuwa mitandao ya kijamii huharibu uelewa wa uhalisia na vile maisha ya wengine yalivyo. Kutokana na watu wengi kupost vitu chanya zaidi kwenye mitandao hutafsiriwa kama mambo yao yako safi kuliko wengine ambao hujikuta wakiwa na huzuni.
Watafiti hao walielezea mitandao ya kijamii kama chombo kinachotoa habari njema zisizo na kikomo zinazoonesha picha za uongo za maisha yaliyohaririwa.