KANYEGELO
JF-Expert Member
- Nov 12, 2019
- 2,293
- 4,969
Hivi kampuni ya Sahara Media Group ndiyo wameshindwa kabisa kufanya maboresho katika king'amuzi chao cha Continental. Namba za simu hazipatikani ofisi pale Rock City Mall wameshafunga.
Vipindi ni vya ovyo ovyo tu , free channel zipo nne tu. Kinaendeshwa kwa ujanja unjanja kutwa kuhama satelite mara amos 5, mara abs2 , mara abs3 mara apostel 75 sasa hivi wapo azer space 2 hivi.
Hizi gharama za kubadilisha mwelekeo wa dish anazilipa nani? Huo msemo, the quality to talk about mbona hauendani kabisa na huduma mnazotoa. Mnadhani wateja wote ni wasabato? Siwaelewi kabisa tuambieni tujue.
Kifurushi kwa mwezi ni Sh 11,999 lakini ni hovyo yaani msipobadilika mtabaki kuwauzia hao wapenda kuangalia makambi. Kuweni na ubunifu. Jifunzeni kwa Azam, Zuku. DStv ndio maana tunashindwa kuthamini vya nyumbani kama mambo ndio hovyo hivyo.
Yaani imekuwa tu bora liende TCRA naomba ingilieni kati katika hili.