-Maswali 50 ya WATANZANIA kwa MZEE LOWASSA..
Baada ya kufuatilia hotuba yako ya ufunguzi wa kampeni za UKAWA jangwani kwa umakini mkubwa, naomba Mzee Edward Ngoyai Lowassa unisaidie mimi na wananchi wenzangu wa TANZANIA kujibu maswali haya;
WANAMABADILIKO;
Watanzania wamechoshwa na Rushwa, wanachukia UFISADI, Mzee unamkakati gani dhidiya wala rushwa na mafisadi..?
MAMA NTILIE;
Kilio chetu ni juu ya mgambo kutusumbua na mazingira mabovu ya biashara,tukakulalamikia bei kubwa ya vyakula na mazao, jibu letu liko wapi..?au atakuja kutujibu Babu Seya ukishamtoa jela..?
MADALADALA;
Mzee tulikubeba kutoka Masaki mpaka Gongo la mboto, njia nzima tukikueleza kero zetu, Hatujakusikia ukisema kitu kuhusu usumbufu wa Traffic na kutunyang'anya leseni zetu..?
WAKAZI WA DAR;
Mzee tumekupa mapokezi ya kufa mtu, lakini unajua kuwa tumeamka saa kumina moja alfajir ili kuwahi mkutano wako wa saa tisa Jangwani, Tatizo la foleni na shida ya Usafiri haujazungumzia kabisa...Mzee umetusahau..?
WANAFUNZI;
Elimu bure kutoka shule ya msingi mpaka chuo kikuu, sawa ila Mzee kwa mapato gani..? Au ndio muendelezo wa maigizo..?
WACHUMI;
Sarafu yetu imeendelea kushuka kwa kasi ya ajabu, imetoka kuwa hela ya madafu imekuwa hela ya pipi, Mzee na hili nalo umelisahau..?
WANASHERIA:
Nini maana ya utawala wa sheria unaouzungumzia..? ipi haki ya watoto waliolawitiwa kinyume na maumbile na Babu Seya na Wanawe, au Mzee unaujua Ukweli ambao hautaki kutuambia..?
WAZANZIBARI;
Ni upi msimamo wako na maoni yako juu ya Katiba inayopendekezwa..kuwa Muwazi..?
MZEE hauoni tofauti ya maisha ya Wazanzibari kabla na baada ya kufungwa kwa Farid na Kundi lake..? Mzee amani imerudi Zanzibar au tuambie mahusiano yako na UAMSHO..?
WAGONJWA;
MZEE watanzania wenzako tunaumwa Mzee..,Nini Hatma ya Afya za Watanzaniaau WEWE mwenzetu sio mgonjwa..?
WANAMABADILIKO;
MZEE tuliahidiwa SLAA atahudhuria jangwani na kuipa nguvu mpya kasi ya mabadiliko, Mzee mlimsahau au ilikuwa ni Changa la macho..?
VIJANA;
MZEE ulisema tatizo la ajira ni bomu, ila hatujakuelewa, ina maana umetuacha tulipuke au mkakati wetu uko kwa Balal..?
WANAKIJIJI;
MZEE umetukomoa au umefanya kwa bahati mbaya kutuwekea hotuba yako kwenye Intaneti, haujui zaidi ya watanzania asilimi 80 hawajui kitu kinaitwa Intaneti..?
WATUMISHI;
MZEE, mishahara yetu haikidhi mahitaji, gharama za maisha ni ghali mno..mbona hatujakusikia ukitutaja, au sisi ni mpango wa kando..?
WACHUMI;
MZEE, nini hatma ya mchumi mwenzetu Prof Lipumba katika genge la wanamabadiliko, au umemchukua TAMBWE Hizza Mhitimu wa darasa la saba kuwa mbadala..?
Inaendelea.....