Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,743
- 25,535
Naombeni niwadokolee machache kumhusu mwalimu ambayo sidhani kama wengi mliyafahamu, na kama wapo ni yale waliyoyafahamu kwa kuyasikia tuu lakini hayajaandikwa popote!.
1.Baba yake alikuwa ni Chifu na alikuwa na wake 22!.
Jee unawafahamu ndugu wengine wa Nyerere kwa Upande wa Baba!. Hawa Julius Kambarage Nyerere (JK-Nyerere), Joseph Kizurira Nyerere (JK Nyerere), na John Kiboko Nyerere (JK Nyerere), hawa ni ndugu wa Tumbo moja. Jee ndugu wengine wa Mwalimu kwa hao wake wengine 22 wa baba yake ni kina nani?.
2.Kumbe Mwalimu alibahatika kusoma kwa bahati tuu!. Ndugu wengine wote kwa Baba, ukiachia wa tumbo la Mama yake, waliishia kuchunga mbuzi!.
Baba yake, alikataa Ukristo kata kata!. Wamishenari walipomshawishi kuachana na dini asili na kujiunga na Ukristo, aliwauliza Ukristo una nini ambacho dini za asili hazina!. Walimjibu, Upendo, Amani, Unyenyekevu, Utii, Haki etc, aliwajibu tena kwa mifano hai jinsi wanavyohubiri Upendo, Amani, Unyenyekevu, Utii na Haki.
3.Alianza shule akiwa na miaka 12, na darasani alikuwa na akili sana hivyo akarushwa baadhi ya madarasa!.
Akiwa Tabora School ndipo alipo pokea Ukristo kwa kubatizwa jina la Julius ambalo alilicopy toka kwa Julius Ceaser!
4.Akiwa Tabora School, alikuwa ni mtoto mkaidi sana!. Adui zake wakuu walikuwa ni viranja!. Alishitakiwa mara kadhaa kwa mwalimu mkuu na ukafikia wakati Mwalimu Mkuu akamaamua Julius afukuzwe shule!. Mwalimu wake wa darasa licha ya utundu wake, alimpenda sana kwa sababu alikuwa na akili sana!. Hivyo akamnusuru kufukuzwa shule kwa kumfanya na yeye awe prefect!.
Source ni Mwalimu Mwenyewe katika mahojiano na mwandishi Mzungu yaliyofanyika mwaka 1964 mara baada ya muungano!.
Jee na wewe, kuna yoyote ya mwalimu unayoyajua na hayaandikwa popote, ungependa ku share na sisi?!.
A Man From Mars
The Monk Who Sold His Ferrari