Usiyayajua kuhusu Somalia

Diwani

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2014
Posts
2,903
Reaction score
3,140
Habari JF

Katika kupitia Hapa na pale kuhusu Mataifa yenye "Foundation" ya African political and social historical background, Nimekutana na Mataifa kama Misri, Ethiopia, Libya, Tunisa pamoja na taifa lingine toka kwenye pembe ya Afrika Somalia, Licha ya umaarufu wa hali yake ya kisiasa iliyodumu muongo mmoja na nusu lakini yafuatayo ni mambo (10) ambayo huenda huyafahamu kuhusu Somalia.

  1. Somalia ni taifa la kwanza Africa kuwa na mapatano ya amani ya kisiasa juu ya utawala baada ya uchaguzi mkuu (Ngazi ya Rais); Baada ya uchaguzi wa Rais, mwaka (1960-1967) raisi wa kwanza wa Somalia, Aden Abdulle Osman Daar aliyeongoza taifa hilo alishindwa uchaguzi na aliyekuwa waziri mkuu wake kwenye serikali yake, Bwana Abdirashid Ali Shermarke, katika uchaguzi wa kidemokrasia. Bwana Daar alikubali kuachia nchi kwa Shermarke Kwa njia amani. Jambo ambalo limekuwa tofauti kwa mataifa mengine Africa
  2. Mogadishu ni mji pekee ulioanzishwa na Waarabu, waajemi na wahindi. Mji wa Mogadishu katika karne ya 10 ulikuwa ni mji pekee Africa wenye ulinzi wa hali ya juu, hata hivyo hadi leo mji huo hautambuliki hesabu yake kamili ya watu, ingawa Meya wa zamani wa jiji hilo Warsame Mohammed Hassan alikadiria idadi ya watu kuwa milioni 3, bila kuwepo na sensa kamili
  3. Mogadishu ni mji pekee duniani ambapo silaha huuzwa sokoni kama bidhaa nyingine; Katika soko kuu la Bakara katika mji huo, silaha huuzwa wazi na wasambazaji maarufu wa jina la Yemeni. Silaha zinazouzwa ni bunduki ndefu za ulinzi "Riffles"
  4. Wasomalia hutumia tuu, huduma yao ya benki itambulikayo kama "Dahabshiil mobile money". Wasomalia huipenda huduma hii na huitumia bila kuhusisha benki nyingine za kimataifa na za Muungano wa benki za wajasiriamali. Dahaabshil ni moja kati ya kampuni kubwa za huduma ya pesa zenye matawi nchi 155 duniani
  5. Somalia ni nchi ya kwanza Mashariki mwa Afrika kuanzisha mahusiano ya kidiplomasia na Uchina mwaka 1960.
  6. Mogadishu ndio mji pekee Afrika wenye pwani na fukwe ndefu, zenye kilomita za mraba 3, 025
  7. Somalia ndio nchi pekee Africa yenye gharama ndogo za utumiaji simu. Kuna makampuni 11 pekee ya simu yaliyounganishwa nchi nzima ikiongozwa na Somalia Telecom, kampuni ya kwanza binafsi ya simu iliyoanzishwa mwaka 1994
  8. Somalia ni nchi ya kwanza Afrika kuanzisha E-passport mwaka 2007. Mwaka 2014, serikali kuu nchini Somalia ilipiga hatua zaidi kuanzisha E-passport mpya zenye ubora wa kimataifa.
  9. Somalia ina mahala pa sanaa ya ujenzi inayofahamika kama Shanghai mjini Mogadishu, eneo ambalo pia lipo nchini Uchina likimaanisha mahala pa sanaa za ujenzi
  10. Somalia ni moja kati ya mataifa yanayosifika duniani kuwa na historia ya uandishi wa mashairi, pia huitwa "Home of poets" na urembo.

chanzo: 10 things you didn't know about Somalia - Africlandpost
 
Kwa kuongezea tu ndani ya somalia kuna serikali au "nchi" tatu ambazo ni Somalia yenyewe, Putland(jimbo) na Somaliland

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna wakati fulani ilikuwa kidogo tu twende huko tulitaka kuingia huko kwa kupitia lamu,kenya badaye bosi wangu mvimba macho machale yakamcheza....

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kuongezea tu ndani ya somalia kuna serikali au "nchi" tatu ambazo ni Somalia yenyewe, Putland(jimbo) na Somaliland

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukizungumzia Somaliland ni Kama una zungumzia Zanzibar na Tanganyika... Uzuri ni kuwa Somali Mogadishu na Somaliland walitawaliwa na na nchi mbili tafauti... Mmoja na Italy mwingine na Britain... Na baada ya Uhuru wakaamua kuungana na kutengeneza Somalia moja... Ila baada ya Somaliland kuona Somali Mogadishu amani hamna wakaamua kuvunja muungano na kujitenga...

Na Somaliland ni sehemu yenye amani usipate kusikia... Hakuna nchi yenye amani naweza sema kama Somaliland...
 
Yaa ni kweli vita wao wanavickia tu kwa majirani zao Somalia. But licha ya muungano kuvunjika bado kuna vitu wanashare nadhani(sna uhakika) wanatumia muundo wa federal government

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…