Usivumilie Dharau

Usivumilie Dharau

Dr leader

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
1,043
Reaction score
1,314
Usiwaamini wanaofanya dharau kuwa jambo la kawaida

Wanapokupotezea — wanadai wako busy.
Wanapokukosea— “human nature.”
Lakini wewe ukifanya hata nusu ya hayo ghafla umebadilika,
Umeanza kiburi,
Wewe ndio tatizo,

Hiyo sio bahati mbaya… hiyo ni tabia yao.
“Watu wengi hawana shida na maumivu ya wengine… wanachukia tu wanapoyapata wao.”

Wanakufanya ulie.
Wanakuumiza huku wanaheka.
Wanakudharau halafu wanaona ni utani tu.

Lakini siku unawarudishia ladha ile ile—
wanaitisha kikao cha dharura kukujadili

“Heshima sio hisia ni mipaka.”
Ukiwa mpole sana, wanakukanyaga.
Ukiwa mvumilivu sana, wanakuzoea.
Ukiwa mzuri kupita kiasi, wanakutumia.

“Usijieleze sana kwa mtu anayejua anachokufanyia.”
Hawa sio wajinga.
Wanajua wanakuumiza.
Wanajua wanakudharau.
Tofauti ni moja tu
wanaamini hutafanya chochote.
Na kwa muda mrefu… ulikuwa sahihi kwao.


✍️Abuuabdillah
 
Mi nishawagundua nawanyoosha haijalishi umri, wakitaka kunifanyia ushenzi wanajua tu huyu hatokubali tumuache!
sipendi ujinga mpaka wamejua!
 
Back
Top Bottom